Michezo

Kocha Ndayiragije Kukifumua Upya Kikosi Taifa Stars
Kocha Ndayiragije Kukifumua Upya Kikosi Taifa Stars

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Etienne Ndayiragije amesema atalazimika kuita wachezaji wapya wa kuunda kikosi cha Taifa Stars mara ratiba mpya itakapotolewa kulingana na uwezo wa wachezaji kwa wakati huo baada ya kuvunja kambi hivi karibuni.

Taifa Stars ilivunja kambi yake ya kujiandaa na mechi ya kufuzu (AFCON) dhidi ya Tunisia pia kujiwinda na michuano ya Ubingwa wa Mataifa Afrika, (CHAN) inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchin mwao pekee kutokana na kuahirishwa kwa michuano yote sababu ya mlipuko ya virusi vya corona duniani kote.

Katkati ya mwezi huu, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) lilisimamisha mechi zote za kufuzu za mashindano ya Afrika kwa ushauri wa Shirika la Afya Dunani (WHO) kwa ugonjwa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya corona.

Mechi zilizofutwa ni za tatu za na za nne kufuzu Fainali za AFCON 2021 ambazo zilipangwa kufanyika kati ya Machi 25 na 31 mwaka huu, kufuzu Fainali za Kombe la Dunia la Wanawake chini ya umri wa miaka 20 zilizopangwa kufanyika kati ya Machi 20 na 22 na marudiano Machi 27 na 29 mwaka huu.

March 24, 2020

Mecky Mexime Atembea na mikataba ya Yanga Mikononi.
Mecky Mexime Atembea na mikataba ya Yanga Mikononi

KOCHA wa Kagera Sugar Mecky Mexime amefichua kwa mara ya kwanza kuwa anatakiwa na klabu ya Yanga ameshapewa mkataba huo tangu mwishoni mwa mwaka jana, lakini kuna baadhi ya vipengele havijakaa sawa hivyo bado hajasaini mkataba huo wala kuurudisha.

Mexime beki na Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Tafa Stars amesema kwamba kuzifundisha timu za Simba, Yanga au Azam ni rahisi sana kuliko vilabu vingine vya Tanzania.

Inaaminika, Mwenyekiti wa Yanga SC, Dk. Mshindo Msolla ni shabiki mkubwa wa Mexime tangu anacheza nafasi za ulinzi klabu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Yanga ilitaka kumpandisha Mkwasa hadi kuwa Mkurugenzi wa Ufundi, lakini ikazimika kumfanya Msaidizi wa Eymael kutokana na Mexime kusita kusaini mkataba.

March 24, 2020

Club ya Mtibwa sugar wapewa jukumu jipya
Club ya Mtibwa sugar wapewa jukumu jipya

UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa kwa sasa wachezaji wanapaswa watulie na familia zao na kutoa elimu kuhusu Virusi vya Corona.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa kwa sasa wamevunja kambi kufuatia agizo la Serikali.

"Tumevunja kambi kutokana na agizo la Serikali kutoruhusu mikusanyiko isiyo ya lazima ili kujikinga na kusambaa kwa Virusi vya Corona, tumewaambia wachezaji kwamba wanapaswa watulie na familia na kutoa elimu bora ya kujikinga na virusi kwani wao ni mabalozi.

"Kwa sasa hatutakuwa na kambi tumeivunja rasmi kila mchezaji ataendelea na ratiba zake akiwa nyumbani, ni matumaini yetu baada ya muda hali itatengamaa na maisha yataendelea," amesema.

March 20, 2020

Kocha wa Yanga "Nilitaka kuja Tanzania miaka minne iliyopita"
Kocha wa Yanga Nilitaka kuja Tanzania miaka minne iliyopita

KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael,amesema kuwa alikuwa ana mpango wa kuja Tanzania miaka minne iliyopita lakini mambo hayakuwa kama alivyotarajia na kupelekea muda huo akabaki Afrika Kusini.

Kwa sasa Eymael anakiongoza kikosi cha Yanga ambacho kinashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara akipokea kijiti cha aliyekuwa Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera ambaye alipigwa chini kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni mwenendo mbovu wa timu.

Eymael amesema :"Nilikuwa nina mpango wa kuja Bongo miaka minne iliyopita kuifundisha Yanga, sababu kubwa nilikuwa napenda kuja Tanzana ila mambo hayakwenda sawa.

"Kwa sasa nipo ndani ya Yanga ninaendelea na maisha na kuna mengi ambayo ninayafanya ila yote kwa yote ninafurahi kuwa Tanzania," amesema Eymael.

Mpaka serikali ya Tanzania inatoa maelekezo ya kusitisha michezo ukiwemo mpira wa miguu, katika ligi kuu mpaka sasa club hiyo ya Yanga ipo nafasi ya Tatu ikiwa na alama zake 51 huku watani wao wa jadi Simba SC wakiongoza ligi kwa alama 71.

March 20, 2020

TFF imemtangaza Mkurugenzi wa Ufundi msomi kuliko wote
TFF imemtangaza Mkurugenzi wa Ufundi msomi kuliko wote

Shirikisho la soka Tanzania TFF leo limetangaza vigezo ilivyovitumia kumuajiri Oscar Mirambo kuwa mkurugenzi mpya wa ufundi wa TFF, Mirambo ambaye ana leseni daraja B ya ukocha kabla ya kutangazwa kuwa mkurugenzi wa ufundi alikuwa kocha.

Mirambo alikuwa kocha msaidizi wa kikosi cha Serengeti Boys kilichoshiriki fainali za mataifa ya Afrika U 2017 nchini Gabon na yale yaliofanyika Tanzania kama mwenyeji alikuwa kocha mkuu licha ya kuwa haikupata matokeo chanya sana, hizi ndio sifa na CV ya Oscar Mirambo zilizotangazwa na katibu jana.

October 18,2019


Radio Uhai 94.1 FM Tabora Sauti ya Tumaini

© Radio Uhai