Habari Za Kitaifa

Mbowe achaguliwa tena kuiongoza CHADEMA
Mbowe achaguliwa tena kuiongoza CHADEMA

Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amechaguliwa tena katika nafasi hiyo baada ya kupata kura 886 sawa na 93.5% dhidi ya mpinzani wake Cecil Mwambe aliyepata kura 59 sawa na 6.2%. Mbowe atatumikia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano. Matokeo hayo yametangazwa leo Alhamisi Desemba 19, 2019 saa 11 alfajiri na msimamizi wa uchaguzi, Sylvester Masinde, akibainisha kuwa kura tatu ziliharibika.

Uchaguzi huo umefanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Baada ya Masinde kumtangaza Mbowe kuwa mshindi, idadi kubwa ya wajumbe wa mkutano mkuu walinyanyuka kwenye viti na kumfuata mbunge huyo wa Hai kwa ajili ya kumpongeza.

Wagombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa (Bara) walikuwa wagombea wawili,Tundu Lissu na Sophia Mwakagenda, Lissu amepata kura 930 sawa na 98.8% huku Mwakagenda (aliyetangaza kujitoa akiwa ukumbini) akipata kura 11 sawa na 1.2%.

December 19, 2019

Rais Magufuli, amezitaka Mahakama kutekeleza wajibu
Rais Magufuli, amezitaka Mahakama  kutekeleza wajibu

Rais Dkt John Magufuli, amezitaka taasisi zinazotoa haki kutekeleza wajibu wao ipasavyo ili kuepuka mlundikano wa mahabusu nchini

Rais magufuli amelitaka jeshi la polisi, jeshi la magereza, ofisi ya mwendesha mashtaka,na ofisi ya mwanasheria mkuu kusaidiana na mahakama kuhakikisha wanafanikisha suala hilo.

Akizungumza katika uzinduzi wa jingo la kisasa la mahakama ya wilaya ya chato na uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha zima moto wilayani humo,ambapo rais magufuli akavitaka vyombo vyote vinavyofanya kazi ya kutoa haki kushirikiana ili kuweza kuondoa murundikano wa mahabusu nchini.

akizungumzia utendaji kazi wa jeshi la zimamoto na uokoaji rais magufuli amelitaka jeshi hilo kuongeza juhudi katika kazi ili kumaliza malalamiko yanayotolewa mara kwa mara dhidi yao.

kwa upande wake jaji mkuu prof ibrahim juma amesema kuwa mahakama inaendelea kutekeleza mpango mkakati wa uboreshaji wa miundo mbinu unaohusisha ujenzi wa majengo pamoja na utoaji wa huduma bora za mahakama,huku kamishena jenerali wa jeshi la zimamoto nchini thobias andengenye akisema ujenzi wa kituo cha zima moto na uhokoaji wilayani chato utaghalimu sh.million mia tisa hadi kukamilika kwake mwezi feb mwakani.

December 19, 2019

Jeshi la polisi lajipanga kudhibiti uhalifu
Jeshi la polisi lajipanga kudhibiti uhalifu

Kamanda wa polis mkoa wa Tabora Barnabas Mwakalukwa amesama jeshi la polisi mkoa limejipanga kudhibiti uhalifu katika kipindi cha sikukuu za krismass na mwakampya.

Kamanda Mwakalukwa amesema jeshi hilo litaimarisha ulinzi kwa kufanya doria za miguu na kuwa kila nyumba ya ibaada itakuwa na ulinzi wa polisi hivyo wananchi wasiogope kuhusu usalama wao.

Amesema ili hali ya usalama itawale wananchi wanawajibu wa kuchukua tahadhari binafsi ikiwa ni pamoja na matumizi sahihi ya vyombo vya usafiri na kuzingatia sheria za usalama barabarani kwa vyombo vyote ambapo pia amepiga marufuku ulipuaji baruti na uchomaji matairi wakati wa kusherehekea.

Aidha mwakalukwa amesema matukio ya ulawiti yameongezeka kutoka matukio 25 kwa mwaka 2018 hadi kufikia matukio 27 kwa mwaka huu ambapo ni ongezeko la asilimia 8 kwa mwaka 2019.

Kwa upande wa Ajali za barabarani mkoani Tabora zimepungua kwa asilimia 78 ikiwa ni juhudi ambazo zimefanywa na jeshi hilo wakishirikiana na wananchi na wadau mbalimbali kwa kutoa elimu ili kuweza kupunguza ajali hizo zinazo ghalimu maisha ya watu.

December 19, 2019

Wanaodhaniwa kula chakula chenye sumu idadi yaongezeka
Wanaodhaniwa kula chakula chenye sumu idadi yaongezeka

watendaji ustawi wa jamii manispaa ya tabora wametakiwa kuwasilisha taarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia kila baada ya miezi mitatu

Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya tabora mjini KOMANYA ERICK KITWALA wakati wa uzinduzi wa kituo cha kusaidia wahanga wa vitendo vya ukatili (one stop center) kilichopo kituo cha afya maili tano.

Bwana kitwala Amesema kila baada ya miezi mitatu kamati ya ulinzi na usalama ya manispaa itakuwa ikipokea taarifa hiyo na kuwataka kuwasikiliza wananchi ikiwa ni pamoja na kutunza siri

Amesema kuwa kituo hicho cha pamoja cha kuhudumia wahanga wa vitendo hivyo na wananchi kwa ujumla wanatakiwa kutoa taarifa huku wakiachana na tabia ya kuwaficha wanaofanyiwa ukatili kwa lengo la kujipatia fedha.

Nae Baraka MAKONA afisa ustawi wa jamii mkoa wa tabora amesema kuwa wamekwisha kuwajengea uwezo watumishi na wataendelea kufanya hivyo ili kuweza kuhakikisha muda wote huduma inapatikana katika kituo hicho.

tabora ni miongoni mwa mikoa mitano inayoongoza hapa nchini kwa vitendo vya ukatili, ambapo mnamo tarehe 10 DECEMBER mwaka huu katika maadhimisho ya siku kumi na sita za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia mkuu wa wilaya ya tabora alihaidi kuanzisha kituo cha pamoja kwa ajiri ya kuhudumia wahanga wa vitendo vya ukatili kwa manispaa ya tabora

December 17,2019

Wanaodhaniwa kula chakula chenye sumu idadi yaongezeka
Wanaodhaniwa kula chakula chenye sumu idadi yaongezeka

Siku moja tangu kuripotiwa kwa Watu 45 kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kufuatia kula chakula kinachodhaniwa kuwa na sumu wakiwa Msibani, Wizara ya Afya imesema idadi ya Watu imeongezeka.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Faustine Ndugulile amesema hadi sasa wamefikia Wagonjwa 53 na bado uchunguzi unaendelea kufanyika kujua kiini cha tatizo.Pia Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto imekanusha taarifa za kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa unaofananishwa na Malaria katika jiji Dar es Salaam.

Naibu waziri wa Wizara ya Afya Dokta Faustine Ndugulile amethitibitisha hayo jijini Dar es Salaam.

Kanusho hilo linakuja kufuatia kuwepo kwa taarifa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusiana na uwepo wa hali ya homa kali,inayoambatana na kukohoa, mafua na maumivu makali ya kichwa kwa baadhi ya watu katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Da es Salaam.

December 17,2019

RC Mwanri apiga marufuku kilimo bila Miti
RC Mwanri apiga marufuku kilimo bila Miti

Mkuu wa mkoa wa TABORA AGREY MWANRY amepiga marufuku kampuni au mtu yeyote kujihusisha na kilimo cha tumbaku iwapo hatakuwa na shamba la miti ya kupandwa ili kulinda mazingira.

Kufuatia zao hilo kuendelea kuzalishwa katika wilaya mbalimbali mkoani Tabora mwanri amewaagiza wakulima na vyama vya msingi kuhakikisha wanapanda miti zaidi ya kuanza shuguli za kilimo ikiwa Ni njia ya kuzuia uharibifu wa mazingira.

Maagizo hayo yametolewa wakati Mwanri akizindua kampeni ya upandaji miti kwa vyama vya msingi wilayani Uyui iliyoandaliwa na kampuni ya JTI.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya UYUI,GIFT MSUYA amesema kumekuwa na changamoto ya miti inayopandwa asilimia kubwa imekuwa ikikauka na akaahidi kuwa serikali ya wilaya hiyo watahakikisha wanasimamia kila mkulima anapanda miti kabla ya kulima.

Kampeni ya upandaji miti kimkoa ilizinduliwa wilayani Kaliuwa na kwa wilaya ya Uyui imezinduliwa katika katika vijiji vya MASWANYA kata ya Malola kwa kupanda miti hekta 1.6 sawa na hekari 4 na MIGUMGUMALO kata ya Usagali kwa kupanda hekta 1.2.

December 17,2019

Polisi Kyela asakwa kwa tuhuma za kumbaka Mwanafunzi
Polisi Kyela asakwa kwa tuhuma za kumbaka Mwanafunzi

Shule zote za msingi nchini Uganda, Januari mwakani zitaanza kufundisha lugha ya Kiswahili na baadae kufanya mitihani kwa lugha hiyo.

Hatua hiyo imeelezwa ni mkakati wa nchi hiyo, kutaka kujitanua katika Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kuona nchi nyingine wanachama wa jumuiya hiyo na nje ya jumuiya zimeitangaza lugha hiyo kuwa rasmi na kuwekwa kwenye mitaala. Mbali na hatua hiyo, Uganda pia imeanzisha Baraza la Kiswahili, huku kikianza kusambaa kwa kasi mashuleni.

Nchi nyingine za Afrika Mashariki ambazo zinakitambua Kiswahili kama lugha rasmi ya taifa ni Tanzania, Kenya na Rwanda, huku Burundi na Sudan Kusini zikiingiza lugha hiyo adhimu katika mitaala yake ya shule. Wizara ya Elimu Uganda imesema nchi hiyo imejiandaa kuanza kufundisha lugha ya Kiswahili shuleni, baada ya kufanyika majaribio na kwamba itaanza kufundishwa kuanzia darasa la nne mpaka la saba.

Kamishna Msaidizi wa Elimu ya Msingi Uganda, Dk Tony Mukasa alisema hayo wakati wa mkutano wa maofisa tawala uliofanyika juzi nchini humo.Alisema tayari wameshambaza vitabu vya Kiswahili shuleni, huku walimu wakiwa wamepata mafunzo katika kipindi cha miaka minne iliyopita."Lengo ni kukukifanya Kiswahili kuwa lugha ya pili ya taifa kutokana na kuwa inatumika kwa kiasi kikubwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki," alisema.

December 10/12/2019

Polisi Kyela asakwa kwa tuhuma za kumbaka Mwanafunzi
Polisi Kyela asakwa kwa tuhuma za kumbaka Mwanafunzi

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ulrich Matei amesema bado wanamsaka Askari Polisi wa kituo cha Polisi Kyela Daniel Mlanda kwa tuhuma za kumbaka na kumpa mimba Mwanafunzi wa kidato cha kwanza Wilayani Kyela na kisha kutoroka, Matei amesema wakimpata atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Licha ya tuhuma za kumpa mimba Mwanafunzi, Askari huyo anadaiwa pia kumzalisha Afisa Mtendaji mmoja na kumtelekeza na Mtoto, pia Mwanafunzi mmoja kutoka Chuo cha Ufundi Kyela anadai kuzalishwa na Askari huyo na kuachwa kwenye mataa licha ya kuahidiwa ndoa hapo awali.

December 10/12/2019

Wafungwa 207 mkoani Tabora wapata msamaha
Wafungwa 207 mkoani Tabora wapata msamaha

Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dk john Pombe magufuli amesamehe wafungwa zaidi ya 5000 wakiwemo wafungwa 207 kutoka mkoani tabora.

Akizungumza katika sherehe za kuadhimisha miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika zilizofanyika hapo jana kitaifa mkoani mwanza rais magufuri amesema mkoa unaongoza kwa wafungwa waliopata msamaha huo kuwa ni mkoa wa kagera .

Amesema kuwa kwa madaraka aliyopewa ibara 45 ibala ndogo ya kwanza kifungu cha a mpaka d ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inampa mamlaka ya kufuta au kusamehe adhabu ya mtu aliyetiwa hatiani na mahakama

kwa upande wake raisi zanzibar dk ally mohamed shein amesema kuwa ili amani iweze kudumu ni kuendelea kuwa na mshikamano na upendo kwa mataifa yote.

nao mawaziri wastaafu awamu zote kuanzia awamu ya kwanza hadi ya nne wamesema watanzania ni vyema kuendelea kuitunza amani iliyopo kwa nguvu zao zote

Tanganyika ilipata uhuru mnamo December 9.1961 huku Zanzibar ikipata uhuru wake 1962.na nchi mbili hizi zikapata kuungana mnamo mwaka 26 april 1964.

December 10/12/2019

Kijana akutwa amekufa katika Eneo la makaburi
Kijana akutwa amekufa katika  Eneo la  makaburi

Kijana mmoja ambae ametambulika kwa jina la Jackson John Mtasha anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 27 Mkazi wa Mtaa wa mihogoni ,amekutwa akiwa amekufa katika Eneo la makaburi ya mihogoni mjini Tabora.

Wakizungumza na radio uhai fm katika eneo la tukio baadhi ya wananchi walioshuhudia maiti ya kijana huyo ,wamesema kuwa tukio hilo limewasikitisha watu wengi wa maeneo hayo ,huku wakiomba serikali kufanya upepelezi wa kina ili kuweza kuwabaini wale wote waliouhusika na tukio hilo na kuwachukulia hatua kali za kisheria.

George Bagem ni Kamanda wa polisi wa wilaya ya Tabora mjini akiwa na mkuu wa upelezi wa wilaya hiyo nao wamefika katika eneo la tukio na kisha kuzungumza na wananchi waliofurika kushuhudia maiti ya kijana huyo ,ndipo wakatoa rai kwa wananchi kuacha tabia za kujichukulia sheria mkononi pindi wanapowakamata wahalifu katika maeneo yao.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Tabora Mjini Komanya Eric Kitwala yeye amekemea tabia za mauji ya ovyo kwa wananchi huku akisema kuwa atakaebainika kuhusika na kifo cha kijana huyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Kwa Mujibu wa Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa serikali ya wilaya ya Tabora ,inapaswa kuanzisha utaratibu wa ulinzi shirikishi kwa wananchi ili kuweza kupunguza matukio ya mauji Hapa Mjini Tabora.

November 8,2019

CHADEMA yatangaza kujitoa katika uchaguzi
CHADEMA yatangaza  kujitoa katika uchaguzi

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza kujitoa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika November 24, mwaka huu. Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ametangaza uamuzi huo leo kwa madai kuwa uchaguzi huo ni batili na wakishiriki watahalalisha ubatili huo.

Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe amatangaza uamuzi huo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ambapo amesema sababu kubwa ni wagombea wa chama hicho kuenguliwa kwa sababu mbalimbali.

Mbowe amesema mara baada ya kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho na wabunge, maazimio waliyokubaliana ni kugomea uchaguzi huo sababu majina ya wagombea wengi kukatatwa.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika Novemba 24, mwaka huu.

November 8,2019

53 wametunukiwa stashahada ya biblia na theolojia
53 wametunukiwa stashahada ya biblia na theolojia

Chuo cha biblia cha western bible college cha mkoani tabora kimefanya mahafali yake ya kwanza ambapo wanafunzi 53 wametunukiwa stashahada ya biblia na theolojia

Akizungumza katika sherehe ya mahafali hayo mgeni rasmi katika hafla hiyo askofu mkuu wa kanisa Tanzania assemblies of god(tag)dkt barnabas mtokambali amewataka wahitimu kujiendeleza zaidi ikiwa ni pamoja na kuwa watumishi wazuri katika shamba la bwana.

Aidha askf mtokambali akieleza kuhusu mafanikio ya kanisa hilo katika kutoa elimu ya vyuo vya biblia nchini amesema zaidi ya wanafunzi elfu 8 wamehitimu ndani ya miaka 10.

Kwa upande wake mkurugenzi wa elimu taifa wa kanisa la tag Jonas mkoba amempongezaaskofu mtokambali kwa maono ya kuanzisha chuo hicho katika mkoa wa tabora kwani kimekuwa msaada wa kiroho na kimwili

Awali Akitoa taarifa ya chuo kwa mgeni rasmi mkuu wa chuo hicho reveland kenned lukilo ametaja mafanikio ya chuo hicho tangu kifunguliwe rasmi mwaka jana 2018 ikiwemo kuanzishwa kwa kanisa la chuo

Wakizungumza na radio uhai fm baada ya kutunukiwa stashahada zao baadhi ya wahitimu wamesema kuwa wako sasa wako tayari kumtumikia mungu sambamba na kufanya kazi kubwa ya kuwaongoza waamini

chuo hicho cha wesrerten bible college(wbc)kinapatikana kata ya ilolangulu mkoani tabora ambacho ni miongoni mwa vyuo vya biblia vinavyomilikiwa na kanisa la Tanzania assemblies of god tag

November 8,2019

Watoto wawili wateketea kwa moto Kagera
Watoto wawili wateketea kwa moto Kagera

Watoto wawili katika kitongoji cha kigema kata ya kishanda wilayani mreba mkoani kagera wamepoteza maisha baada ya kuteketea kwa moto uliosababishwa na kibatari wakati walipokuwa wamelala kwenye nyumba

Akizungumza na vyombo vya HABARI ofisini kwake kamanda Wa POLISI mkoani kagera kamishina msaidizi wa polisi revocatus malimi amewataja marehemu hao kuwa ni jackson kelvin mwenye umri Wa miaka minine na jovinatha kelvin mwenye mwaka mmoja.

kamanda malimi amesema kuwa Moto huo uliwateketeza watoto hao majira ya SAA nne usiku wakati mama yao aliye tajwa kwa jina la salome kelvin alipokuwa ameenda sokoni kununua chakula

Aidha kamanda malimi amewaomba wazazi na walezi mkoani kagera kuwa waangarifu kwa watoto ili kuepukatana na majanga yoyote ambayo yanaleta athari kwa jamii

October 22/2019

Wananchi Tabora wahofia mafuriko
Wananchi Tabora wahofia mafuriko

Wananchi wa kata ya maroro mtaa wa kombo masai Tabora manispaa wameiomba serikali kuwatatulia kero ya miundo mbinu ya barabara pamoja na mitaro ili kuepukana na adha ya mafuriko pale mvua zitakapo anza kunyesha .

Wananchi hao wameyasema hayo mara baada ya kutembelewa na redio uhai fm na kujionea hali halisi ya miundo mbinu ya barabara ikiwa ni kipindi cha kuelekea masika na kuimba serikali kuwatatulia tatizo hilo

Akielezea suala hilo mwenyekiti wa mtaa wa kombo masai Rajabu Isike amesema kuwa yeye kama mwenyekiti ameshirikiana na wananchi katika kuchangishana fedha na kujitolea katika kuchimba baadhi ya mitaro

October 22/2019

Mkuu wa Mkoa aagiza Mwalimu kufikishwa mahakamani
Mkuu wa Mkoa aagiza Mwalimu kufikishwa mahakamani

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amewaagiza wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Rukwa kuhakikisha Mkuu wa Shule ya Sekondari Mzindakaya iliyopo kata ya Kaengesa, Wilayani Sumbawanga Dastan Mlelwa anafikishwa mahakamani baada ya kuwabaka na kuwatia mimba wanafunzi wawili wa kidato cha pili na cha tatu katika shule hiyo.

Amesema kuwa anataarifa kuwa mwalimu huyo tayari amekwishajisalimisha katika mikono ya polisi na hivyo kumtaka kamanda wa polisi mkoa, Kamanda wa TAKUKURU mkoa pamoja na Mkuu wa Usalama wa mkoa kufuatilia jambo hilo ili mwalimu huyo asitoke kwenye mikono ya polisi bali apelekwe mahakamani.

Katika hatua nyingine bwn.Wangabo amewaagiza wajumbe hao wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa kufuatilia kesi ya wizi wa mifugo inayomhusisha Afisa mifugo wa mji mdogo wa laela, wilayani Sumbawanga Emanuel Tluwey baada ya kukamatwa akiwa anachinja ng’ombe wa wizi kesi ambayo ilifikishwa polisi na kuonywa kuwa kesi hiyo isifinyangwe finyangwe ili mwizi huyo asichukuliwe hatua.

October 22/2019

Upelelezi wa kumchoma moto mkewe wakamilika
Upelelezi wa kumchoma moto mkewe wakamilika

Upelelezi wa kesi inayomkabili mfanyabiashara Khamis Said, anayedaiwa kumuua na kisha kumchoma na moto wa magunia mawili ya mkaa mke wake Naomi Marijani, na kisha mabaki ya mwili huo kwenda kuyafukia shambani kwake Mkuranga umekamilika.

Akizungumza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Wakili wa Serikali Wankyo Simon, amesema kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekwishakamilika na kwamba upo katika hatua za mwisho za uchapishwaji ili jalada hilo lipelekwe Mahakama Kuu.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mkuu wa Mahakama hiyo Salumu Ally, aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 4, 2019.

Mshtakiwa huyo anadiwa kutenda kosa hilo Mei 15, 2019, nyumbani kwake maeneo ya Gezaulole Kigamboni.

October 22/2019

Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na mvua yaongezeka
Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na mvua yaongezeka

Jeshi la Polisi nchini Tanzania limesema,idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini imeongezeka na kufikia watu 29 kutoka 11.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Edward Bukombe ameliambia Shirika la Utangazaji nchini Tanzania (TBC) kuwa watu 18 wameaga dunia katika mafuriko yaliyotokea katika wilaya za Korogwe, Handeni, Kilindi na Pangani yaliyosababishwa na mvua kubwa katika siku mbili zilizopita mkoani humo.

Ameongeza kuwa, mvua hizo na mafuriko zimeharibu miundombinu na mashamba ya kilimo, na kwamba sekta ya uchukuzi imeathiriwa pakubwa katika mkoa huo.

Jumanne iliyopita, polisi ya Tanzania ilisema watu 11 wakiwemo wanafunzi watano wamefariki dunia kutokana na mvua kubwa zilizonyesha mkoani Morogoro.

Maeneo mengi nchini kwa sasa yanashuhudia mvua kubwa huku mamlaka ya Hali ya Hewa ikiendelea kutoa tahadhari ya kuendelea kwa mvua hizo.

Serikali imewaonya na kuwataka wananchi wanaoishi katika maeneo ya mabonde kuhama maeneo hayo hasa wakati huu ambapo nchi inashuhudia mvua kali ili kuepuka maafa zaidi.

October 18, 2019

Chanjo ya surua- rubella na polio kutolewa bure
Chanjo ya surua- rubella na polio kutolewa bure

Mkuu wa Mkoa wa Tabora AGGREY MWANRI ameagiza vituo vyote vya Afya vilipopewa dhamana ya kutoa chanjo ya surua- rubella na polio kutoa huduma hiyo bure.

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kampeni ya chanjo hiyo ya watoto wenye umri chini ya miaka5 akiwa mgeni rasmi, katika zahanati ya Town clinic manispaa ya Tabora.

Aidha mganga mkuu wa mkoa Tabora DKT HONORATHA RUTATINISIBWA ametoa ufafanuzi juu ya chanjo hizo ambazo zitatolewa na amesema matarajio kwa mkoa mzima ni watoto laki 4 elfu 89 na193 kwa chanjo ya surua- rubella na watoto laki 2 elfu 13 na144 kwa chanjo ya polio.

Kampeni ya chanjo ya surua rubela na polio imezinduliwa rasmi tarehe 17 october 2019 na Waziri wa Afya maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto UMMY MWALIMU Mkoani morogoro ambapo itaendelea mpaka tarehe 21 octoba mwaka huu ikilenga kuwafikia watoto wenye umri wa chini ya miaka 5.

October 18, 2019

Wachimbaji wadodo wadogo waomba msaada
Wachimbaji wadodo wadogo waomba msaada

Wachimbaji wadodo wadogo wa dhahabu wilayani nzega mkoani tabora wameiomba serikali kuwawezesha kupata mitambo itakayo wasaidia kuchimba madini hayo kwa njia za kisasa na kuiahidi serikali kulipa kodi kwa uaminifu

Hayo yamesemwa na wachimbaji hao ambao wamechoka kuchimba dhahabu kwa kutumia masururu na kuiomba serikali iwasaidie kununua mitambo hiyo

Naye Mkuu wa Wilaya ya nzega bwn Godfrey ngupula amesema atashughulikia suala hilo kwa haraka ili wachimbaji hao wanufaike .

October 18, 2019

RC Tabora aendesha zoezi la kuwabaini wavunjifu wa amani
RC Tabora aendesha zoezi la kuwabaini wavunjifu wa amani

Mkuu wa mkoa wa tabora Agrey Mwanry ameendesha zoezi la kuwabaini wavunjifu wa amani ambapo katika wilayani uyui zoezi hilo limezinduliwa kwenye kata ya mabama huku na diwani wa kata hiyo na mchungaji wa kanisa wakiongoza kwa kura za uhalifu.

Wakati akielezea utaratibu wa kuwabaini wahalifu Mwanri amelipatia jina zoezi hilo kama oparesheni fukua fukua ambapo utaratibu unaotumika ni wananchi kuwapigia kura za siri wale wanaodhaniwa kuhusika na matukio ya uvunjifu wa amani.

Gift Msuya mkuu wa wilaya ya Uyui ameendesha zoezi la kuhesabu kura zilizopigwa ambapo diwani wa kata hiyo Akawa ni miongoni mwa waliopigiwa kura na mchungaji wa kanisa kuibuka kinara kwa kura 19

Aidha kamanda wa polis mkoa wa Tabora Barnabas Mwakalukwa amesema vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na baadhi ya watu havitavumilika nabadala yake wahusika watashughulikiwa Zoezi la kuwabaini wahalifu mkoa wa Tabora limeendelea jana september 17 katika halmashauri ya wilaya ya Kaliwa

September 18/2019

Boti yawaka moto ikiwa na abiria 56
Boti yawaka moto ikiwa na abiria 56

Boti ndogo inayofanya safari zake kutoka Bandari ya Kemondo iliyopo Wilaya ya Bukoba kuelekea Kisiwa cha Bumbile kilichopo ndani ya Ziwa Victoria imewaka moto ndani ya maji ikiwa na abiria 56

akizunguza baada ya ajari hiyo kamanda wa polisi mkoani kagera revocatus malimi amesema chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana na watu watatu ambao wamepata majeraha wapo hospitali kwa matibabu zaidi

kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Kagera brg.jeneral gaguti amesema kuwa wananchi wanaosafiri kwa kutumia usafiri wa majini ni vyema kuchukua tahadhari mapema kutokana na ajari ikiwa ni pamoja na kutumi9a maboya yanayoweza kuwasaidia wasizame endapo chombo hicho kikipata ajari .

mikali dominicki ni moja kati ya abiria ambao walikuwemo katika boti hiyo ambapo amesema kuwa alijitosha kwenye maji ili wasiweze kuungua moto

September 18/2019

Walimu mkoani Tabora kupoteza Imani na MCB
Walimu mkoani Tabora kupoteza Imani na MCB

Baadhi ya walimu mkoani Tabora wameeleza kupoteza Imani na benki ya walimu nchini MCB wakidai kutoridhishwa na utendaji wa benki hiyo hasa pale wanapohitaji kuhudumiwa na banki hiyo kama wanachama wake.

hayo yameelezwa Wakati benki ya walimu nchini MCB ikiwa katika utekelezaji wa kampeni yake iliyopewa jina la Amsha amsha iliyofanyika wilayani Tabora mkoani Tabora iliyolenga kuwahamasisha walimu walejee kuitumia benki hiyo.

Wakizungumza wakati wa kampeni hiyo ya Amsha Amsha iliyowakutanisha viongozi wa chama cha Waalimu ngazi za wilaya pamoja na baadhi ya maafisa kutoka benki ya MCB Peter Sizya ni Mwalimu wa shule ya msingi Bombamzinga amesema ni wakati wa benk kuwajibika ili kufikia malengo yake.

Richard Makungwa ni mkurugenzi mtendaji wa benki ya walimu nchini Sanjali ambaye amekiri mapungufu kadhaa katika benki hiyo ya MCB ametoa wito kwa walimu kushirikiana na benki.Aidha mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ameitaka benki ya Walimu nchini MCB kufanya kazi kwa ushindani ili kuwavutia wateja wengi zaidi.

September 18/2019

Waziri mkuu Majaliwa hajaridhishwa na gawio la sh milioni 800
Waziri mkuu Majaliwa hajaridhishwa na gawio la sh milioni 800

WAZIRI MKUU Kassimu Majaliwa amesema hajaridhishwa na gawio la sh milioni 800 linatolewa na kiwanda cha Sukari cha Kilombero ambacho uzalishaji wake ni kikubwa ikilinganishwa na kiwanda cha sukari cha Moshi TPC ambacho kinatoa gawio la sh. billion 15 kwa mwaka.Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Septemba 17, 2019) wakati alipotembelea kiwanda hicho, akiwa katika siku ya nne ya ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro. Amevitaka viwanda vya sukari nchini kuzaliza sukari ya kutosha ili kukidhi mahitaji.

Akizungumzia kuhusu vibali vya uagizaji wa sukari, Waziri Mkuu amesema Serikali iliamua kutoa nafasi ya kuagiza sukari kwa wenye viwanda ili kuepuka ujanja uliokuwa ukifanywa na baadhi ya wafanyabiashara ambao walikuwa wakiagiza sukari kutoka nje ya nchi ambayo nyingine ilikuwa haina ubora.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Tanzania bado kuna uhitaji mkubwa wa sukari hususani ya viwandani, hivyo kusababisha Serikali kutoa vibali kwa wamiliki wa viwanda kuagiza sukari kutoka nje ya nchi. “Viwanda vya ndani vya sukari vihakikishe vinaongeza uzalishaji wa sukari ya viwandani ili kukabiliana na upungufu uliopo.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba amesema mahitaji ya sukari kwa mwaka huu nchini yameongezeka hadi kufikia tani 710,000 ikilinganishwa na tani 610,000 za mwaka jana.

September 18/2019

Tabora yatenga hekar 42 elfu na 53.71
Tabora yatenga hekar 42 elfu na 53.71

Serikali imesema mkoa wa Tabora umetenga hekar 42 elfu na 53.71 katika halmashauri zote nane za mkoa huo ili kutekereza agizo la serikali la kutenga maeneo ya uwekezaji huku halmashauri ya Tabora manispaa ikiongoza kwa kutenga eneo kubwa.

Taarifa hiyo imetolewa bungeni jijini Dodoma kwa niaba ya waziri mkuu wakati likijibiwa swari la mbunge wa viti maalumu Mwanne Mchemba alipotaka kufahamu mikakati ya serikali kuelekeza nguvu katika kuwekeza mkoani Tabora.

September 12/2019

Omari Rashid Nundu (71) amefariki dunia
Omari Rashid Nundu (71) amefariki dunia

Aliyewahi kuwa Waziri wa Uchukuzi katika Serikali ya awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete, na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Simu Mawasiliano Tanzania (TTCL), Omari Rashid Nundu (71) amefariki dunia wakati akiwa njiani akipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa ajili ya matibabu.

Taarifa iliyotolewa leo mchana na Kitengo cha Mawasiliano cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imeeleza kuwa, Nundu alifikishwa hospitalini hapo kwa gari binafsi la kubeba wagonjwa.

Taarifa hiyo imethibitishwa na afisa uhusiano wa muhimbili bi Sophia mtakasimba ambapo amebaisnisha kuwa marehemu alifikwa na umauti kabla ya kufika hospitalini hapo.Juni 12, 2019, Rais wa Tanzania, John Magufuli alimteua Dk Nundu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania ikiwa ni utekelezaji wa makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya Bharti Airtel International.

Katika makubaliano hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania pamoja na ofisa mkuu wa ufundi wanapaswa kuteuliwa na Serikali.Kabla ya Dk Nundu kuteuliwa alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).Wakati huo huo taasisi ya moi imesema hali ya askofu mkuu wa jimbo kuu katolik ds mhashamu yuda tadeo rwaich imeimarika na ufahamu wake umerudi

September 12/2019

Dkt. Ndunguru ateuliwa kuwa mwenyekiti wa (LATRA)
Dkt. Ndunguru ateuliwa kuwa mwenyekiti wa (LATRA)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. John Stanslaus Ndunguru kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA).Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Ndunguru umeanza tarehe 09 Septemba, 2019.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Prof. Antony Manoni Mshandete kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA).

Prof. Mshandete ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma, Utafiti na Ubunifu), Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) kilichopo Mkoani Arusha.

September 12/2019

Kiongozi wa mbio za mwenge akataa Mradi
Kiongozi wa mbio za mwenge akataa Mradi

kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifajohn mkongea ally amekataa kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami wilayani igunga mkoani tabora baada ya kukagua na kugundua kuwa sampili ya nondo hazikupelekwa maabara kupimwa ili kujua ubora wake .

pia kiongozi huyo ametoa wiki mbili kwa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa takukuru wilayani igunga ili kufanya uchunguz wa kina kuhusu utekelezaji wa mradi huo ili kama kuna ubadhirifu wa fedha hatua zaidi ziweze kuchukuliwa .

kabla ya kukataa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara hiyo kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa john mnkongea ally kwa kushirikiana na wenzake walikagua barabara pamoj a na nyaraka mbalimbali za utekelezaji wa mradi huo

mwenge wa uhuru umepokelewa mkoani tabora tayari kwa ziara ya kuzindua kuweka mawe ya msingi na kutembelea miradi 38 yenye thamani zaidi ya shilling billion 16.

baada ya kupokelewa wilayani igunga tayari umekimbizwa katika wilaya iogunga nzenga mji na ambapo kwa tabora manispaa itakuwa tarehe 1 mwezi wa 9 mwaka huu.

mbio za mwenge kimkoa zitadumu kwa muda wa siku nane mkoani hapa ambapo mbio hizo zitahitimishwa wilayani sikonge tarehe 2 mwezi wa 9 mwaka huu.

August 28/2019

Lori la mafuta lapinduka na kumwaga mafuta
Lori la mafuta lapinduka na kumwaga mafuta

Lori la mafuta limepinduka na kumwaga mafuta Alfajiri ya jana Agosti 27, 2019 katika eneo la Michungwani wilayani Handeni.

Jeshi la Polisi limefanikiwa kufika eneo la tukio na kutawanya watu waliokuwa wameanza kukusanyika kuchota mafuta.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Tanga, Solomon Mwangamilo amewataka wananchi kuacha tabia hiyo na kuwataka wawe kwa kwanza kutoa msaada na si kuiba.

Kwaupande wake mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Handeni ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo Godwine Gondwe amesema kama viongozi wa serikali wamesimama katika nafasi zao na kuhakikisha usalama unatawala na kutotokea madhara yoyote.

August 28/2019

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu yapongezwa
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu yapongezwa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameipongeza Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kazi nzuri ya kuchunguza sampuli mbalimbali, kusimamia sheria za usimamizi wa kemikali na kudhibiti vinasaba vya binadamu.

Rais Magufuli ametoa pongezi hizo jana alipotembelea Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali iliyopo Kivukoni Jijini DSM ambapo ameona jinsi mitambo ya uchunguzi vya kisasa inavyofanya kazi ikiwemo uchunguzi wa vinasaba vya miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali ya moto iliyotokea Mjini Morogoro tarehe 10 Agosti, 2019 baada ya lori lililobeba mafuta kupinduka na kisha kulipuka moto.Akiwa katika maabara hiyo rais magufuli ameshuhudia mashine mpya za uchunguzi zinavyofanya kazi

Rais magufuli ameeleza kuwa hatua hiyo madhubuti ni za kuimarisha Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kununua vifaa vipya na vya kisasa, kuongeza wafanyakazi na kuibadili kutoka kuwa Wakala wa Serikali na kuwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kutambua umuhimu wake mkubwa

August 21,2019

Afariki dunia baada ya kusadikiwa kujinyonga
Afariki dunia baada ya kusadikiwa kujinyonga

Mtu mmoja amefariki dunia baada ya kusadikiwa kujinyonga katika kijiji cha Saitabau kata ya Saitabau halmashauri ya wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa arusha Jonathan Shanna amemema tukio hilo limetokea hapo jana Tarehe 19.08.2019 muda wa saa 4 usiku katika kijiji cha Saitabau kata ya Saitabau halmashauri ya wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha.

Kamanda shana amemtaja aliyefariki katika tukio hilo kuwa ni rehema eliudi (31) mwarusha,mfanyabiashara mkazi wa kijiji cha saitabau na kwamba alikutwa ndani ya chumba chake akiwa amefariki dunia.Aidha kamanda shanna ameeleza kuwa wanamshiklilia mme wa marehemu anaitwa julias kabola kwaajili ya uchunguzi zaidi

August 21,2019

Akutwa kwenye paa la nyumba ya Mchungaji
Akutwa kwenye paa la nyumba ya Mchungaji

JESHI la Polisi Mkoa wa Iringa linamshikilia na kumhoji mwanamke Kabula Masunga(41), anayedaiwa kufanya ushirikiana baada yakukutwa kwenye paa la nyumba ya Mchungaji Jeremia Charles saa 11 alfajiri.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Juma Bwire amesema leo Agosti 20,2019 kuwa mwanamke huyo anatuhumiwa kufanya ushirikina huo eneo la Isele Ilula wilayani Kilolo mkoani Iringa na kusababisha taharuki kwa wakazi wa maeneo hayo.

Amefafanua mwanamke huyo ambaye ni mpagani na mkazi wa Morogoro alikutwa akiwa katika mazingira hayo akiwa amejifunga mavazi ya rangi nyekundu na nyeusi lakini kifua aliacha wazi."Pia alikutwa akiwa na ungo uliyofungwa kitambaa ya rangi nyeusi na nyekundu.Amekutwa pia na pembe la ng'ombe na alijifunga hirizi mikononi.

Mwanamke huyo alikuwa na wenzake wanne inaodaiwa alikuwa anasafiri nao kwa kutumia ungo.Kamanda Bwire amesema kwa sasa wanaendelea kumhoji zaidi ili kufahamu lengo la kufanya ushirikina huo.

August 21,2019

Mbaroni kwa mauaji ya Mama wa miaka 55
Mbaroni kwa mauaji ya Mama wa miaka 55

Jeshi la Polisi Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora limewakamata Watu watatu na kuwafikisha Mahakama ya Wilaya ya Igunga kwa tuhuma za mauaji ya Mama wa miaka 55, Veronica Makumbi, baada ya kumtuhumu kuwa ni Mchawi

Watuhumiwa hao wanadaiwa kumuua mwanamke huyo July 28 mwaka huu saa 6:30 usiku.Waliokamatwa ni Sung'hwa Ngasa, Willson Sunhnwa na Sunhwa Zumbi wakazi wa kitangili.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Elimajid Kweyamba, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Igunga, Lydia Ilunda, alidai washtakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 196 kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya 2002.

Kesi imeahirishwa hadi Agosti 29, itakapotajwa tena na washtakiwa walipelekwa mahabusu na hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo..

August 20/2019

Wananchi wapewa wito kushirikiana na polisi
Wananchi wapewa wito kushirikiana na polisi

Kamanda mpya wa jeshi la polisi mkoa wa Tabora Kamishna msaidizi wa polisi Barnamas mwakalukwa ametoa wito kwa wananchi na viongozi mkoani Tabora kushirikiana na jeshi hilo katika kupambana na uhalifu

Ameyasema hayo wakati wa hafla maalum ya kujitambulisha kwa wadau wa usalama mkoani iliyofanyika katika bwalo la polisi jioni ya jana aug 18 2019

Kmanda huyo mpya aliyehamishiwa tabora hivi karibuni amesema ushirikiano kati ya viongozi,wananchi na jeshi hilo ndio sialaha tosha ya kupambana na uhalifu kikamilifu

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tabora Agrey Mwanry amesema kuwa yuko tayari kushirikiana na jeshi la polisi katika kuhakikisha kuwa uhalifu unakomeshwa mkoani Tabora,huku mkuu wa mkoa wa tabora komanya eric akitoa rai kuchukuliwa hatua viongozi wazembe

Hata hivyo baadhi ya wageni waalikwa katika hafla hiyo diwani wa kata ya mtendeni bwn kapela pamoja na mfanyabiashara bwn Vimajo wamemempongeza kamanda mpya pamoja na mkuu wa mkoa wa tabora kwa hatua wanazozifanya kuimarisha usalama

August 20/2019

Idadi ya waliofariki katika ajali ya Moto yafikia 97
Idadi ya waliofariki katika ajali ya Moto yafikia 97

Idadi ya waliofariki katika ajali ya Lori iliyotokea mkoani Morogoro imezidi kuongezeka na kufikia 97 baada ya majeruhi wawili kati ya 20 waliokuwa wamelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam kufarikii dunia.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano MNH, Aminiel Aligaesha amesema majeruhi waliobaki hospitalini hapo ni 18 ambao wote wapo kwenye chumba cha uangalizi maalum (ICU).

Amewataja waliofariki ni Rosijo Mollel (35) aliyefariki juzi Jumapili mchana na Neema Chakachaka ambaye amefariki alfajiri ya jana Jumatatu.

August 20/2019

Rais wa jamhuri ya Afrika Kusini atua Tanzania
Rais wa jamhuri ya Afrika Kusini atua Tanzania

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania john magufuri amempokea rais wa jamhuri ya afrika kusini Ramaphosa na kufanya mazungumzo naye ikuru jijini dares salam ambayo yamelenga zaidi katika kuimarisha ushirikiano katika Nyanja za kibiashara na uwekezaji Rais ramaphosa yupo nchi kwa ziara ya kikazi ya siku mbili

Akizungumza muda mfupi baada ya kumalizika kwa mazungumzo hayo rais magufuri amesema afrika kusini imepiga hatua kubwa katika ukuaji wa uchumi na ni nchi ya kumi na tatu kwa uwekezaji hapa nchini hivyo ametumia nafasi hiyo kumuomba mh raisi ramaphosa kuhamasisha wawekezaji kutoka afrika kusini kuja kuwekeza hapa nchini katika maeneo mbalimbali ikiwemo viwanda vya dawa na vifaa tiba ,kilimo na utalii.

Aidha marais wa pande zote mbili awamezungumzia ukuaji wa biashara baina ya nchi hizo mbili ambao umekuwa ukiongezeka huku Tanzania ikiombwa ushirikiano zaidi na kubadilishana uzoefu katika sekta ya utalii madini ambapo afrika kusini imeahidi kuendelea kuimarisha lugha ya Kiswahili.

August 16,2019

Kardinali Polycarp Pengo ameng’atuka
Kardinali Polycarp Pengo ameng’atuka

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kardinali Polycarp Pengo ameng’atuka wadhifa huo na nafasi yake imechukuliwa na Askofu Mkuu mwandamizi, Yuda Ruwa’ichi wa Jimbo kuu la Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu (TEC), Charles Kilima, Askofu Pengo ameng’atuka baada ya kuomba kustaafu majukumu ya kuliongoza Jimbo Kuu la Dar es Salaam ombi lililoridhiwa na Baba Mtakatifu Francisko na kumteua Askofu Ruwa’ichi kushika nafasi hiyo. Askofu Pengo ameliongoza Jimbo Kuu la Dar es Salaam kwa miaka 27 tangu mwaka 1992 akimpokea Askofu Laurean Rugambwa.kumpongeza Kardinali Polycarp Pengo, Askofu mkuu Mstaafu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam kwa huduma yake makini kwa watu wa Mungu nchini Tanzania. Amesimama kidete kulinda imani, maadili, umoja na mshikamano wa watanzania.

August 16,2019

Majeruhi saba kati 32 wamefariki dunia
Majeruhi saba kati 32 wamefariki dunia

Majeruhi saba kati 32 wa ajali ya lori la mafuta ya petroli iliyoanguka na kulipuka mkoani Morogoro waliokuwa wakitibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam nchini Tanzania wamefariki dunia.

Hii ina maana kuwa waliofariki kutokana na ajali hiyo iliyotokea Jumamosi iliyopita ya Agosti 10, 2019 eneo la Msamvu mkoani Morogoro hadi kufikia asubuhi ya leo Alhamisi Agosti 15,2019 ni 89.

Akitoa taarifa hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano (MNH), Aminiel Aligaesha amesema kwa sasa wamebaki majeruhi 25 kati ya 46 waliopokelewa hospitalini hapo kutoka Hospitali ya Rufaa ya Morogoro.

Amesema kati ya majeruhi hao 16 wapo katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) huku wengine tisa wakiendelea kupatiwa matibabu katika wodi maalum iliyotengwa kwa ajili ya majeruhi hao.

August 16,2019


Radio Uhai 94.1 FM Tabora Sauti ya Tumaini

© Radio Uhai