Habari Za Kitaifa

Spika Wa Bunge Amtaka Mbowe Kurejesha Fedha alizochukua na Kutomjibu Rais Katika Hotuba zake
Spika Wa Bunge Amtaka Mbowe Kurejesha Fedha alizochukua na Kutomjibu Rais Katika Hotuba zake

Spika wa Bunge, Job Ndugai amemtaka Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kurejesha fedha alizopewa na Bunge ili kuhudhuria vikao vya Bunge lakini hakuhudhuria.

Mei 18, 2020, Jijini Dodoma wakati akizungumza na vyombo vya habari Spika Ndugai amesisitiza kuwa, lazima fedha hizo zirejeshwe na kumtaka Freeman Mbowe asiwapelekeshe wabunge wake .

Amesema baadhi ya wabunge wa chama hicho waliyopaswa kurudisha fedha walizochukua tayari wamerejesha na wengine bado hawajarejesha na Freeman Mbowe pia bado hajarejesha huku akimtahadharisha kuacha kujibu hotuba za kiongozi wa nchi.

“Walio wengi wamerudisha lakini wengine bado akiwemo yeye Mheshimiwa Mbowe na ndo ubaya wangu unapokuwa hapo nichukue nafasi hii kumwambia milioni mbili na elfu 40 lazima arudishe ni taratibu za kifedha, mimi kusimamia taratibu za kifedha ni wajibu wangu.

"Atumie nafasi yake ya kiongozi wa upinzani bungeni kushauri na siyo kuropoka, sehemu yake sahihi ni bungeni na siyo sehemu nyingine. Mbowe kama kiongozi wa upinzani bungeni anapewa ofisi, secretary, mhudumu, dereva, gari, nyumba, marupurupu, posho, senior officer, Sasa anachotaka kingine ni nini? Yaani yeye kila kitu anapinga, hiyo siyo sawa, namsihi aache.

Aidha, Spika wa Bunge Job Ndugai amesema Rais Magufuli atahitimisha Bunge Juni 16,2020 jijini Dodoma badala ya Mei 29,2020 iliyopangwa awali ili kufuata kalenda ya usomaji bajeti ya Jumuia ya Africa Mashariki.

Mwenendo wa wabunge wa chama cha Democrasia na Maendeleo baada ya kauli ya mwenyekiti wao ya kujiweka karantini umejenga taswira tofauti ikiwamo ya wabunge kuvuliwa uanachama nawengie kutangaza kuachana na chama hicho akiwemo mbunge wa Kilombero Peter Lijualikali aliyetangaza kuachana na chama hicho bungeni may 18 mwaka huu.

May 19, 2020

Magari kutoka Kenya mpaka wa Horohoro Kuzuiwa kuingia Tanzania
Magari kutoka Kenya mpaka wa Horohoro Kuzuiwa kuingia Tanzania

Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigella ameziagiza mamlaka zote zilizopo katika mpaka wa Horohoro mkoani Tanga kutoruhusu gari lolote kuingia nchini kutoka nchini Kenya.

Shigella ametoa kauli hiyo mara baada ya kutembelea eneo hilo na kukuta baadhi ya madereva wa Kitanzania wakiwa katika eneo hilo kwa zaidi ya siku sita bila ya kuruhusiwa kuingia upande wa Kenya.

Amesema kwa magari yoyote yanayotoka nchi za Rwanda ,Burundi nan chi ambazo italazimu kupita mpaka huo yaruhusiwe kupita kwa kufuata taratibu zilizopo.

Aidha ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya mpaka huo ili kuzuia watu wanaoingia nchini kinyume cha sheria.

May 19, 2020

Tanzania Yafungua Rasmi Anga, Safari za ndege ruksa Kupita na Kutua
Tanzania Yafungua Rasmi Anga, Safari za ndege ruksa Kupita na Kutua

Tanzania imetangaza rasmi kufungua anga lake nakuwa ndege zote zikiwemo za watalii na kibiashara zipo huru kuingia Tanzania.

Waziri wa ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano Mh.Isack Kamwelwe amezungumzia suala hilo jijini Dodoma na ameliagiza Shirika la ndege Tanzania (ATCL) kujipanga ili kurejesha Huduma za usafiri kwa nchi ambazo zimefungua Anga zao.

“Baada ya tathmini ya mwenendo wa ugonjwa huo hapa Tanzania kama ilivyoelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jana mai 17, 2020, imebainika kuwa udhibiti wa ugonjwa huo umeendelea kuimarika

” Kwamba wagonjwa wamekuwa wakipungua katika vituo mbalimbali vya afya nchini hivyo Serikali inatangaza kufungua anga lake rasmi kuanzia jumatatu tarehe 18, mei, 2020″ amesema Kamwelwe.

Amesema kuanzia sasa ndege zote za kibiashara, misaada, kidiplomasia , dharura na ndege maalumu zinaruhusiwa kuruka, kutua, na kupita juu ya anga la Tanzania kama ilivyokuwa awali.

May 19, 2020

Waziri wa Viwanda Awahaikikishia Wananchi Upatikanaji wa Sukari
Waziri wa Viwanda Awahaikikishia Wananchi Upatikanaji wa Sukari

Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa (Mb), leo tar. 14 Mei, 2020 ametembelea shehena ya awali ya tani 600 ya sukari iliyopokelewa katika bandari ya Mwanza.

Waziri Bashungwa amewahakikishia wananchi kuwa Sukari iliyoingia nchini na kusambazwa Mikoa mbalimbali ya Nchi inaenda kumaliza changamoto ya upatikanaji wa Sukari.

Katika ziara hiyo waziri Bashungwa amewaagiza wakuu wa mikoa yote nchini kuhakikisha sukari inauzwa kwa bei elekezi iliyotangazwa na serikali huku akiahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria wafanyabiashara watakaopandisha bei.

Wiki kadhaa katika mioka mbalimbali nchini kumekuwa na hali ya kupanda kwa bei ya sukari tofauti na bei elekezi ya serikali hali iliyoashiria uhaba wa bidhaa hiyo nchini.

May 14, 2020

Jeshi la Polis Tabora Kuwakamata Watoto Wahalifu Bila kujali Umri wao
Jeshi la Polis Tabora Kuwakamata Watoto Wahalifu Bila kujali Umri wao

Jeshi la polisi mkoani tabora limesema halitasita kuwachukulia hatua wanafunzi wanaotumiwa kwa vitendo vya uharifu wakati huu wakiwa nyumbani kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa corona.

Akizungumza na waandishi wa habari jumatano mei 13, Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora ACP. Barnabas Mwakalukwa amesema baadhi ya wahalifu wanaokamatwa ni vijana wenye umri chini ya miaka 18.

“Tumegundua vijana wengi wameacha kufanya shughuli zao za kusoma na wameanza kufanya vitendo vya uhalifu, tutaendelea kuwakama hata kama ni mototo mdogo sisi tutawakama ”

Kamanda mwakalukwa AMESEMA mara baada ya uchunguzi kukamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani

Mwakalukwa Amewataka Wananchi Kutokufanya Uhalifu Kwa Kisingizio Kuwa Wakati Huu Wa Corona huku wakidhani Jeshi La Polisi Halifanyi Kazi,Wao Wako Kazini Kama Kawaida.

May 14, 2020

Serikali ya Tanzania yakanusha taarifa za kufungwa kwa mpaka wake na Zambia.
Serikali ya Tanzania yakanusha taarifa za kufungwa kwa mpaka wake na Zambia.

Serikali imewatoa hofu Watanzania na kusema kwamba Zambia haijafunga mpaka wake na Tanzania na kusisitiza kuwa uhusiano kati ya nchi hizo ni mzuri.

Tamko hilo limetolewa kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, ametoa ufafanuzi huo jana mei 13, Bungeni jijini Dodoma, wakati akihitimisha hoja za Wabunge waliojadili Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

" Nataka niwaambie Zambia haijafunga mpaka na Tanzania, narudia tena Zambia haijafunga mpaka na Tanzania ,haya si maneno yangu,ninayo barua kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje nchini Zambia Joseph Malanji ambaye Mungu amemjaalia kujua lugha nyingi.

"Kwa hapa Tanzania anazungumza kinyakyusa , Kinyiha, Kinyamwanga, na jana na leo tumezungumza kwa Kiswahili. Naomba nisome barua yake japo ni jambo ambalo si la kawaida , ameniandikia barua ambayo imefika leo baada ya kufanyika kwa mazungumzo,"alisema Profesa Kabudi na kisha kuisoma barua hiyo iliyoandikwa kwa lugha ya Kingereza.

Profesa Kabudi alifafanua kwa mujibu wa barua hiyo ambayo imefafanua kwa kina kuwa Zambia haijafunga mpaka, imeeleza kuwa Kamati ya timu ya watalaamu kutoka Tanzania na Zambia watakutana kwa pamoja kuweka mambo sawa na kisha huduma kurejea kama kawaida.

May 14, 2020

Wizara ya Ardhi Kutenga Hekari 234,349 Ujenza Wa Viwanda Nchi Nzima
Wizara ya Ardhi Kutenga Hekari 234,349 Ujenza Wa Viwanda Nchi Nzima

Wizara ya ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi imesema imetenga jumla ya hekari laki mbili na themanini na nne elfu,mia tatu arobaini na tisa nukta saba kwa ajili ya ujenzi wa viwanda katika miji mbalimbali nchini.

Hayo yamebainishwa mei 11 jijini Dodoma wakati bunge likiendelea kujadili bajeti ya wizara ya aridhi,nyumba na maendeleo ya makazi ambapo amesema vipaumbele kwa mwaka 2020/2021 ni ujenzi wa viwanda ambavyo tayari maeneo yametengwa.

Aidha waziri lukuvi amesema kwa sasa wizara inatekeleza tangazo la serikali za kuanzisha ofisi za ardhiri katika kila mkoa ili kumsogezea mwananchi huduma karibu

baadhi ya wabunge wameiomba wizara hiyo kushughulikia migogoro ya aridhi kushughulikiwa nchini.

May 12, 2020

Mkuu wa Mkoa Wa Tabora aja na “Opareshen Bamiza” Kwa Madereva Na Abiria Wasiyovaa Barakoa
Mkuu wa Mkoa Wa Tabora aja na “Opareshen Bamiza” Kwa Madereva Na Abiria Wasiyovaa Barakoa

Mkuu wa mkoa wa Tabora amezindua rasmi oparesheni itakayosaidia Abiria katika vyombo vya usafiri kuchukua tahadhari dhidi ya janga la virusi vya Corona.

Oparesheni hiyo imezinduliwa baada ya makubaliano kati ya madereva, vyombo vya usalama na mkuu wa mkoa Aggrey Mwanri katika kikao cha pamoja kilichofikia muafaka na oparesheni hiyo kupewa jina la “Oparesheni Bamiza”

Akisoma tamko la MADEREVA mbele ya mkuu wa mkoa ALLY ATHUMANI MWAKILISHI WA CHAMA CHA MADEREVA TABORA amesema wamekubaliana na maazimio yaliyowekwa katika kikao hicho,hivyo watachukua taadhari zote na dhamana ya kuwalinda abiria watakaotumia vyombo vyao vya usafiri.

Baada ya kupokea tamko la madereva, mkuu wa mkoa Aggrey Mwnri akaeleza msimamo wa serikali kwa atakayekiuka makubaliano hayo.

Katika kikao hicho jeshi la polisi na vikosi vya usalama barabarani mkoa wameahidi kutekeleza maelekezo yote na kuitendea kazi ipasavyo oparesheni hiyo.

May 12, 2020

Wabunge Wane CHADEMA Wafukuzwa Uanachama, Spika Ndugai Asema bado ni Wabunge Halali
Wabunge Wane CHADEMA Wafukuzwa Uanachama, Spika Ndugai Asema bado ni Wabunge Halali

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetanganza kuwafukuza uanachama Mbunge wa Rombo Joseph Selasini na Mbunge wa Moshi Vijijini Anthony Komu kwa kuwa wamepoteza sifa ya kuwa wanachama wa chama hicho.

Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika ametangaza uamuzi huo jumatatu mei 11 yakiwa ni matokeo ya kikao cha Kamati Kuu ya chama.

“Mbunge David Silinde na Wilfred Rwakatare sio tu wamekiuka agizo la Chama bali wamekuwa wakijitokeza kwenye vyombo vya habari kutoa maneno ya kashfa na kejeli dhidi ya maagizo ya Chama na Viongozi wa Chama, Kamati Kuu CHADEMA imefikia uamuzi wa kuwafuta uanachama

Kufukuzwa uana chama kwa wabunge hao ni kutokana na madai ya kukiuka maagizo yaliyotolewa na mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe ya kuwataka wabunge wa CHADEMA kutohudhuria vikao vya bunge ili kujikinga na CORONA.

Wabunge wengine waliofukuzwa uanachama nipamoja na Wilfred Lwakatare mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini na David Silinde.

Baada ya Taarifa ya Chadema kwa wabunge hao Spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Joab Ndugai amesema licha ya taarifa hizo za kwenye mitandao lakini bado anawatambua kuwa ni wabunge halali kwakuwa viongozi hao wa chama hawana mamlaka ya kuwaondoa wabunge aliowaapisha.

May 12, 2020

Tabora Yazindua Mpango wa Elimu kwa njia ya Vyombo vya Habari Kulinda Elimu Kwa watoto
Tabora Yazindua Mpango wa Elimu kwa njia ya Vyombo vya Habari Kulinda Elimu Kwa watoto

Serikali ya mkoa wa Tabora imezindua mpango wa masomo ya wanafunzi kwanjia ya vyombo vya habari ili kuwalinda kitaaluma wanafunzi katika kipindi ambapo shule zimefungwa

Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri, amezindua mpango huo katika kikao na madiwani wa kata pamoja na watendaji wa manispaa ya Tabora ambapo amesema mpango huo unalenga kuwawekea mazingira ya kielimu watoto wanapokuwa nyumbani baada ya shule kufungwa kuepuka kusambaa kwa virusi vya Corona.

Amesema kufungua mpango huo mkoani Tabora utasaidia familiya nyingi hasa maeneo ya vijijini ambazo hazina uwezo wa kunufaika na elimu kwa njia ya televisheni kupata huduma hiyo kupitia redio zilizopo mkoani humo.

Akikabidhi mpango huo ulio ambatana na ratiba za masomo hayo afisa elimu mkoa wa Tabora Mwl. Michael Ndigola amesema kuwa mpango huo umeandaliwa kwakuhusisha wataalamu wa habari pamoja na wataalamu wa teknolojia hivyo utakuwa msaada mkubwa kwa watoto kujifunzia.

May 7, 2020

Mbunge Wa Jimbo La Kishapu Akamatwa Na Silaha 10 Na Risasi 536 Bila Ya Kuwa Na Vibali Halali Vya Umiliki.
Mbunge Wa Jimbo La Kishapu Akamatwa Na Silaha 10 Na Risasi 536 Bila Ya Kuwa Na Vibali Halali Vya Umiliki.

Mbunge wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga Suleiman Masoud Nchambi (CCM) anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma ya kukutwa na silaha 10,risasi 536 na nyama zinazodhaniwa ni za wanyamapori kilo 35 kinyume na sheria.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga (ACP) Debora Magiligimba amethibitisha kukamatwa kwa Mbunge huyo na kusema kuwa tukio hilo limetokea Mei 3 mwaka huu majira ya saa sita usiku katika mtaa wa Lubaga Manispaa ya Shinyanga.

Amesema kuwa Jeshi la Polisi lilifanikiwa kukamata silaha hizo baada ya kufanya upekuzi katika nyumba yake na baaada ya kupata taarifa za kiintelijensia kuwa Mbunge huyu anajihusisha na uwindaji haramu katika eneo la Negezi kwa kutumia gari lake aina ya Nisan hard body lenye namba za usajili T 760 DSD.

Amefafanua kuwa Nyama hizo zimepelekwa katika maabara ya mkemia mkuu wa Serikali kwa uchunguzi na gari hilo limekamatwa na Mtuhumia atafikishwa Mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

May 7, 2020

Baraza la Madiwani Kalambo Kuwapeleka Mahakamani watendaji waliokula pesa
Baraza la Madiwani Kalambo Kuwapeleka Mahakamani watendaji waliokula pesa

Spika wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai Mei 6, 2020 amewataka wabunge wa Chadema waliosusia vikao vya bunge kwa kisingizio cha Corona kurudi haraka bungeni

Spika ndugai amesema endapo watakaidi agizo hilo la kurudi bungeni basi itawalazimu siku watakayo rudi wawe na cheti kinachoonesha kuwa wamepima ugonjwa wa Corona na majibu yake na kurudisha pesa walizolipwa ambazo ni posho za vikao la sivyo hatua zaidi zitachukuliwa.

"Wabunge hawa ambao ni watoro walipokuwa wanaondoka walilipwa fedha za kuanzia Mei 1 - 17 Jumla ya zaidi Sh Mil 110, nawaagiza kuanzia Freeman Mbowe kurudisha Tsh Mil 2 na elfu 40 na wenzake wote hao, huu ni utoro wa hiari kwa lugha rahisi huu ni wizi na wale wengine wamelipwa Mil 3 warudishe" amesema Spika Ndugai.

Aidha Spika Ndugai amekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kujiandaa kulipa gharama za kesi iliyofunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho,Tundu Lissu baada ya mahakama kutupilia mbali kesi hiyo.

May 7, 2020

Baraza la Madiwani Kalambo Kuwapeleka Mahakamani watendaji waliokula pesa
Baraza la Madiwani Kalambo Kuwapeleka Mahakamani watendaji waliokula pesa

Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Daudi Sichone ametangaza kuwafukuza kazi pamoja na kuwapeleka mahakamani watendaji wa vijiji wanaokusanya mapato na kutowasilisha mapato hayo benki kwaajili ya utekelezaji wa matumizi mbalimbali ya halmashauri hiyo.

Amesema kuwa tabia hiyo ilianza kwa watendaji wachache kutumia fedha wanazokusanya hali iliyopelekea na watendaji wengine kuiga tabia hiyo na matokeo yake kuwa desturi kwa watendaji hao kutumia fedha za makusanyo huku ikisomeka kuwa ni wadaiwa (defaulters) jambo ambalo Mwenyekiti huyo analipinga na kusema watendaji hao sio wadaiwa bali ni wezi wa fedha za halmashauri na hivyo wachukuliwe hatua kama wezi.

“Imekuwa Shida, kuna watendaji ambao sasa hivi wanaona kuwa TAKUKURU nako ni kama nyumbani, na sisi njia nyingine ambayo tunayo, nguvu yetu tuliyonayo ni ya kuwafukuza tu na kuwapeleka mahakamani, kwasababu hatuna namna, tumewapeleka kwenye vyombo ambavyo ndio tunavitegemea, zimefanya kazi yake kwa nguvu zote, tumekwenda hivyo lakini…” Alisema.

Aliongeza kuwa kuna baadhi ya watendaji wadaiwa ambao wameshajiandikisha ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kalambo ili ifikapo tarehe 30.05.2020 wawe wamemaliza kulipa fedha hizo na kushauri kuwa watendaji hao wasisubiriwe hadi ifike tarehe hiyo, kwani kuna watendaji ambao madeni yao ni makubwa na hivyo hawataweza kulipa fedha hizo kwa pamoja na kuitaka ofisi hiyo kuweka utaratibu wa watendaji hao kulipa kidogokigdogo.

Maamuzi hayo yalifikiwa na Mwenyekiti huyo baada ya kukubaliana katika vikao vya kamati ya fedha, Uongozi na Mipango jambo ambalo liliungwa mkono na waheshimiwa madiwani wote waliohudhuria katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo tarehe 2.5.2020 kilichohusu utekelezaji wa hoja za ukaguzi na mapendekezo ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali nchini.

Hadi kufikia tarehe 23.04.2020 halmashauri za Mkoa wa Rukwa zinadai zaidi ya shilingi milioni 928 za makusanyo ambayo hayajawasilishwa benki kutoka kwa watendaji, huku halmashauri ya Wilaya ya kalambo ikiwa ya pili kwa kudai ambapo watendaji wake wanadaiwa shilingi 260,496,059 na madiwani wa halmashauri hiyo wakidai zaidi ya shilingi milioni 80.

May 4, 2020

TANZIA.Mchungaji Drt. Peter Mitimingi Afariki Dunia
TANZIA.Mchungaji Drt. Peter Mitimingi Afariki Dunia

Mchungaji kiongozi wa Kanisa la Warehouse Christian Center(WHC), Dkt. Peter Mitimingi amefafiki usiku wa kuamkia leo. Mchungaji Msaidizi wa kanisa hilo Samwel, amethibitisha.

Mpaka anafariki alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma ya the Voice of Hope Ministry, Mshauri wa Saikolojia wa BLCCC.

Alifahamika zaidi kwa mahubiri na mafundisho yake kuhusu mahusiano na maisha ya ndoa yaliyoenea zaidi kupitia Mitandao ya Kijamii.

May 4, 2020

Rais Magufuli Ashangazwa Majibu ya Maabara ya Kupima Corona, Papai Na Mbuzi Sampuli zakutwa na Maambukizi
Rais Magufuli Ashangazwa Majibu ya Maabara ya Kupima Corona, Papai Na Mbuzi Sampuli zakutwa na Maambukizi

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameeleza kuwa na mashaka na majibu yanayotolewa na maabara ya taifa ya upimaji sampuli za virusi vya Coona.

Hali hiyo inajili baada ya kupima sampuli zisizo za binadamu na majibu kuonesha kuwa kunamaambukizi ya virusi hivyo.

Rais Magufuli ameyasema hayo may 3, 2020 katika hafla fupi ya kumwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Augustine Mahiga aliyefariki dunia.

“Tulipeleka Sample ya Ndege Kware ilikuwa Positive, Mbuzi akawa Positive, Kondoo akawa Negative, ukishaona sampo ukamwambia huyu ni binadamu halafu ana Corona maana yake Mapapai yote yangewekwa Isolation.

"Tulipopeleka sampo ya Papai tukaipa jina la Elizabeth (26) Papai lile lilikuwa Positive kwamba lina Corona, maana yake maji ya Papai ni Positive.

”Tulichukua sampo za Mbuzi, Kondoo, Papai, Oil ya gari tukavipeleka maabara na tukazipa majina, mfano Oil tuliipa jina la Jabir Hamza (30), ili leta Negative, sampo ya Fenesi tuliipa jina la Sarah Samweli (45), matokeo inconclusive.

Baada ya hali hiyo Rais Magufuli ameagiza kuchunguzwa mienendo ya maabara hiyo kuwa huenda kunaudanganyifu unaoendelea.

“Kama tunapeleka sampuli za wanyama zinakutwa Positive inawezekana wafanyakazi wa Maabara wanatumika na Mabeberu, kama mapapai, mbuzi yana corona WHO wanapaswa kufanya kazi kubwa ya ziada, kwa hili lililotokea lazima kuna Watu wameambiwa wana corona wakati hawana

Mpaka Rais Magufuli anatangaza hali hiyo Taifa la Tanzania linarekodi kuwa na jumla ya wagonjwa 480 kutokana na taarifa iliyotolewa na wazirimkuu Kassim Majaliwa.

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameeleza kuwa na mashaka na majibu yanayotolewa na maabara ya taifa ya upimaji sampuli za virusi vya Coona.

Hali hiyo inajili baada ya kupima sampuli zisizo za binadamu na majibu kuonesha kuwa kunamaambukizi ya virusi hivyo.

Rais Magufuli ameyasema hayo may 3, 2020 katika hafla fupi ya kumwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Augustine Mahiga aliyefariki dunia.

“Tulipeleka Sample ya Ndege Kware ilikuwa Positive, Mbuzi akawa Positive, Kondoo akawa Negative, ukishaona sampo ukamwambia huyu ni binadamu halafu ana Corona maana yake Mapapai yote yangewekwa Isolation.

"Tulipopeleka sampo ya Papai tukaipa jina la Elizabeth (26) Papai lile lilikuwa Positive kwamba lina Corona, maana yake maji ya Papai ni Positive.

”Tulichukua sampo za Mbuzi, Kondoo, Papai, Oil ya gari tukavipeleka maabara na tukazipa majina, mfano Oil tuliipa jina la Jabir Hamza (30), ili leta Negative, sampo ya Fenesi tuliipa jina la Sarah Samweli (45), matokeo inconclusive.

Baada ya hali hiyo Rais Magufuli ameagiza kuchunguzwa mienendo ya maabara hiyo kuwa huenda kunaudanganyifu unaoendelea.

“Kama tunapeleka sampuli za wanyama zinakutwa Positive inawezekana wafanyakazi wa Maabara wanatumika na Mabeberu, kama mapapai, mbuzi yana corona WHO wanapaswa kufanya kazi kubwa ya ziada, kwa hili lililotokea lazima kuna Watu wameambiwa wana corona wakati hawana

Mpaka Rais Magufuli anatangaza hali hiyo Taifa la Tanzania linarekodi kuwa na jumla ya wagonjwa 480 kutokana na taarifa iliyotolewa na wazirimkuu Kassim Majaliwa.

May 4, 2020

Waziri mkuu Majaliwa Aagiza kushusha bei ya Sukari
Waziri mkuu Majaliwa Aagiza kushusha bei ya Sukari

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataka wafanya biashara kutopandisha bei ya bidhaa na kuwaagiza wakuu wote wa mikoa kufanya ziara za mara kwa mara kwenye masoko na maduka.

Waziri Majaliwa amesema kuwa kumekuwepo kupanda kwa bei ya sukari na amewaagiza wafanyabiashara kushusha bei kwani sukari ipo ya kutosha na amewataka wakuu wa mikoa kuwachukulia hatua kari kwa wale ambao hawatashusha bei ya sukari.

" Natoa wito kwa wafanyabiashara kuhakikisha vyakula muhimu vinauzwa kwa bei ya kawaida, wakuu wa mikoa na wilaya wafanye ukaguzi wa mara kwa mara kwenye masoko ili kuhakikisha bei ni ile ile" Waziri Majaliwa.

“Hakuna haja ya sukari kupanda kuliko ile bai yake ya kawaida bei itaendelea kuwa ile ile ninawaagiza wakuu wa mikoa, yeyote atakayeuza kilo kwa shilingi 4500 chukua hatua kali dhidi yake” -

April 22, 2020

Mahabusu Wapungua Gerezani Hawafanyi Uhalifu Wakiogopa Corona
Mahabusu Wapungua Gerezani Hawafanyi Uhalifu Wakiogopa Corona

Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora limesema matukio ya uhalifu mitaani yamepungua kwa kiasi kikubwa katika wilaya zake kufuatia misako ya polisi inayoendelea usiku na mchana ikiwa ni pamoja na vibaka kuhofia kuambukizwa Corona.

Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora limesema kutokana na kupungua kwa uhalifu katika maeneo mbalimbali ya mkoa huu kumepelekea kupungua kwa mahabusu katika vituo vya polisi ikiwa ni hatua ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona katika mahabusu za polisi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Kamishina Msaidizi wa Polisi Barnabas Mwakalukwa amesema ili kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona katika jeshi hilo limeweka mikakati ya kukagua kambi za asakari na familia zao mara kwa mara kama hatua za kukabiliana na virusi vya corona.

Aidha jeshi la polisi mkoa wa Tabora limetoa onyo kwa wa halifu watakao bainika kutanjwa na wananchi kuwa bado wanaendelea na vitendo vya uhalifu jeshi hilo halitasita kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Katika mkoa wa Tabora taasisi mbalimbali zinachukua tahadhari ya Corona kwa wafanyakazi wake kwa kufuata maelekezo ya watalamu wa afya ikiwa ni pamoja na kuzuia wananchi kuingia katika ofsi zao bila kuwa wamevaa barakoa.

April 22, 2020

Wagonjwa Wa Corona Wafikia 284 Tanzania
Wagonjwa Wa Corona Wafikia 284 Tanzania

Waziri Mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema, hadi Aprili 21, 2020 jumla ya Wagonjwa 284 wamethibitika kuwa na Virusi vya Corona.

Majaliwa amesema Wagonjwa 256 wanaendelea vizuri, 7 wako kwenye uangalizi maalum, 11 wamepona na 10 wamefariki dunia.

Waziri Mkuu ameyasema hayo Jumatano April 22, 2020 akiwa kwenye Maombi ya kuombea Taifa dhidi ya ugonjwa wa covid 19 katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es salaam.

Aidha, Waziri Mkuu amesema jumla ya watu 2,815 waliokuwa karibu na Wagonjwa wamefuatiliwa afya zao ambapo kati yao, watu 1733 hawana maambukizi na watu 12 walikutwa na virusi hivyo (wapo kwenye orodha ya watu 284)

Jumatatu April 20, 2020 Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alitoa taarifa kuwa jumla ya visa vya wagonjwa wa Corona ilikuwa 254 baada ya Wagonjwa 84 kuongezeka.

April 22, 2020

TAKUKURU TABORA WAREJESHEA MALI WAALIMU WASTAAFU WALIOTAPELIWA KWA MIKOPO FEKI
TAKUKURU TABORA WAREJESHEA MALI  WAALIMU WASTAAFU WALIOTAPELIWA KWA MIKOPO FEKI

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa mkoa wa Tabora imefanikiwa kuwarejeshea fedha tasilimu na nyumba zao walimu wastaafu wawili waliotapeliwa kwa mikopo isiyo halali(MIKOPO UMIZA).

Akitoa taarifa ya utekelezaji kwa kipindi cha January –march kwa vyombo vya habari, mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Tabora Bw, Musa Chaulo amesema kiasi cha pesa iliyorejeshwa ni shilingi million 41 na laki mbili .

Pia chaulo amesema nyumba ya mwalimu mstaafu wilaya ya Kaliua wameikabidhi kwa muhusika na nyumba ya pili wameikabidhi kwa mwalimu mstaafu wilaya ya Sikonge yenye thamani ya shilingi milioni kumi na tano

Katika taarifa nyingine Bw Chaulo amsema taasisi hiyo imefanikiwa kurejesha shilling million moja zilizolipwa kwa ajili ya ukarabati wa kisima katika kituo cha afya TUTUO wilayani Sikonge HUKU miongoni mwa kesi zilizofunguliwa na kushinda ni pamoja na kesi ya mhudumu wa afya katika hospitali ya kitete aliyeomba rushwa ili mgonjwa aweze kupatiwa damu.

April 16, 2020

Tanzania yathibitisha wagonjwa wapya 29 wa Corona
Tanzania yathibitisha wagonjwa wapya 29 wa Corona

Wizara ya Afya april 15 imethibitisha uwepo wa wagonjwa 29 wapya waliopata maambukizi ya CoronaVirus, na kufikisha idadi ya watu 88 kutoka 53 waliopata maambukizi ya virusi hivyo.

Wizara ya Afya

April 16, 2020

Serikali Kuajiri Watumishi Wapya Zaidi ya 44,000
Serikali Kuajiri Watumishi Wapya Zaidi ya 44,000

Serikali inatarajia kuajiri watumishi wapya 44,811 katika mwaka wa fedha 2020/2021.

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika ameyasema hayo Jumatano Aprili 15, 2020 wakati akiwasilisha bajeti yake.

Ametaja ajira hizo mpya kuwa ni kada ya elimu (13,529), afya (10,467), kilimo, mifugo na uvuvi (2,145) Jeshi la Polisi (2,725), magereza (685), Jeshi la zimamoto (501), uhamiaji (495) na hospitali za mashirika ya kidini na hiyari (1,262).

Aidha, amesema Serikali inatarajia kuajiri watumishi 13,002 wa kada nyingine zikiwamo za wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma nchini.

Mkuchika amesema pia Serikali itawapandisha vyeo watumishi 222,290 wa kada mbalimbali kulingana na maelekezo yatakayotolewa.

April 16, 2020

Waziri Mkuu wa Tanzania Apokea Msaada wa Sh. Milioni 500 Kukabili Corona
Waziri Mkuu wa Tanzania Apokea Msaada wa Sh. Milioni 500 Kukabili Corona

WAZIRI MKUU amepokea hundi ya mfano ya sh. milioni 500 kutoka kampuni ya Export Trading Group (ETG) zikiwa ni msaada kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa homa ya mapafu unaotokana na maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19) nchini.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea msaada huo Jumanne, Aprili 14, 2020 ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma, kutoka kwa Mkurugenzi mkazi wa ETG, Bw. Nilladri Chowdhury aliyefuatana na maafisa uhusiano wa kampuni hiyo, Bw. Frank Mtui na Bi. Fatma Salum Ally.

“Kwa niaba ya Rais wetu, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli tunawashukuru kwa msaada huu ambao utaisadia Serikali kupunguza makali ya kuwahudumia wananchi wetu. Tunahitaji kuungwa mkono na wadau wengine kama ninyi,” amesema.

Mapema, akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kampuni ya ETG, Bw. Mahesh Patel, Mkurugenzi Mkazi wa ETG, Bw. Nilladri Chowdhury amesema wameamua kuchangia ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika vita ya kupambana na ugonjwa huo.

April 14, 2020

Tanzania wagonjwa wa Corona Wafika 46
Tanzania wagonjwa wa Corona Wafika 46

Wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto nchini Tanzania imetangaza kuongezeka kwa wagonjwa wapya wa virusi vya Corona nakufanya idadi ya waliobainika kufikia 46.

Taarifa ya waziri wa afya Ummy Mwalimu iliyotolewa april 13 mwaka huu imeeleza kuwa wagonjwa wapya 14 ni watanzania na kati yao wagonjwa 13 ni kutoka jijini Dar es salaam na mmoja ni kutoka Arusha.

Taarifa inaeleza kuwa wagonjwa hao wote wanaendelea na matibabu chini ya Uanalizi wa wataalamu.

Ikumbukwe kuwa siku chache zilizopita serikali ya mamlaka ya usalama wa anga nchini Tanzania imetangaza kufuta safari zote za ndege za abiria za kimataifa huku taifa likiwa na rekodi ya wagonjwa saba waliopona corona.

April 14, 2020

Askari auawa na watu wasiojulikana na mwili wake kutupwa kwenye mtaro
Askari auawa na watu wasiojulikana na mwili wake kutupwa kwenye mtaro

Askari wa kituo cha Polisi Kia wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, Sajenti Juma Ango anadaiwa kuuawa na watu wasiojulikana na kutupwa mtaroni karibu na mgahawa wa chakula Bora mita chache kutoka kituo cha Polisi Hai Mjini.

Mwili wa askari huyo aliyekuwa kitengo cha upelelezi kituo cha polisi Kia ulikutwa ukiwa na jeraha kubwa kisogoni na damu zikiwa zimetapakaa usoni.

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya alisema April 14 saa mbili asubuhi watu waliokuwa wakifyeka majani kandokando ya Barabara Kuu ya Arusha Moshi ndio waliouona mwili huo na kutoa taarifa polisi.

“Taarifa zinasema alikuwa na askari wenzake juzi Jumapili ya Pasaka hadi saa nane usiku maeneo ya Msami Baa. “alisema Sabaya

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Salumu Hamduni alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba upelelezi haujakamilika na pindi utakapokamilika taarifa kamili zitatolewa.

April 14, 2020

IGP Sirro: Tumeimarisha hali ya usalama kufuatia vurugu zinazoendelea nchini Msumbiji
IGP Sirro: Tumeimarisha hali ya usalama kufuatia vurugu zinazoendelea nchini Msumbiji

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amesema kuwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini vimejipanga vyema kuhakikisha vinadhibiti vitendo vya uhalifu hasa kutokana na vitendo vya vurugu vinavyoendelea katika nchi jirani ya Msumbiji.

IGP Sirro amesema hayo alhamisi April 9, 2020 wakati akizungumza na baadhi ya wakazi wa eneo la Mnazi Mmoja mkoani Lindi, nakuwataka wananchi hao wajikite katika shughuli halali za kujiletea maendeleo.

Aidha,IGP Sirro, amewataka Watanzaania hususan vijana kuacha kutumiwa na watu wachache wanaowataka wajiingize kwenye vitendo vya uvunjifu wa amani nchini ikiwemo kufanya uhalifu.

April 9, 2020

Waziri Jafo awasilisha makadirio ya bajeti 2020/2021 TAMISEMI
Waziri Jafo awasilisha makadirio ya bajeti 2020/2021 TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo ameliomba bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha kiasi cha shilingi Trioni 7.02 kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu katika mwaka wa fedha 2020/2021.

Akiwasilisha hoja hiyo april 8 2020,Bungeni Jijini Dodoma Mhe Jafo amesema makadirio hayo yanahusisha Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-(OR-TAMISEMI), Tume ya Utumishi wa waalimu, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Akifafanua zaidi waziri Jafo amesema kiasi cha shilingi Trilioni 3.8 kitatumika kwa ajili ya mishahara, Bilioni 851 kwa matumizi mengine na kiasi cha shilingi trilioni 2.29 kitatumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Aidha waziri Jafo amesema katika mwaka wa Fedha wa 2020/2021 Serikali imepanga kutumia shilingi bilioni 42.3 kwa ajili ya ujenzi wa maabara za sekondari ambazo zitajengwa katika kila Halmashauri.

April 9, 2020

Waziri wa Afya Awataka Viongozi wa Dini Waepushe Misongamano Kwenye Nyumba Za Ibada Ili Kukabiliana na Corona
Waziri wa Afya Awataka Viongozi wa Dini Waepushe Misongamano Kwenye Nyumba Za Ibada Ili Kukabiliana na Corona

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametoa rai kwa viongozi wa dini nchini kuhakikisha wanaepuka misongamano kwenye nyumba za ibada hasa katika kipindi hiki cha sikukuu ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona.

Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam Alhamisi Aprili 9, wakati wa kikao cha kitaifa cha viongozi wa dini kilichozungumzia jinsi ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona.

"Ugonjwa tumeletewa kutoka nje, hivi sasa takwimu za jana, juzi na wiki iliyopita tumeanza kuambukizana wenyewe kwa wenyewe. viongozi wangu wa dini naomba niliweke wazi it’s no longer imported cases, tumeanza local transmission.

Waziri Ummy amewaomba viongozi hao kuhakikisha waumini wenye dalili za kikohozi, mafua na homa wanabaki nyumbani.

Amesema hadi sasa Tanzania kuna idadi ya wagonjwa 25 na taarifa nyingine ataitoa mchana baada ya kupata maelezo watalaamu waliopo maabara.

April 9, 2020

Tanzia: Katibu mkuu wa CUF Khalifa Suleiman Khalifa afariki dunia
Tanzia: Katibu mkuu wa CUF Khalifa Suleiman Khalifa afariki dunia

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Khalifa Suleiman Khalifa amefariki dunia usiku wa kuamkia Jumanne Machi 31 2020 akipatiwa matibabu katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam. .

Mwanaye Said Khalifa amesema tangu Januari 2020 kwa nyakati tofauti baba yake aliugua na kulazwa katika hospitali hiyo.

Machi 16, 2019 Khalifa akichaguliwa na baraza kuu la uongozi la CUF kuwa katibu mkuu wa pili wa chama hicho akichukua nafasi ya Maalim Seif Sharif Hamad ambaye alivuliwa uanachama.

March 31, 2020

Mgonjwa wa corona Afariki Nchini Tanzania
Mgonjwa wa corona Afariki Nchini Tanzania

Waziri wa Afya maendeleo jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu amesema ameeleza kutokea kifo cha kwanza kwa mgonjwa wa COVID 19 chini Tanzania.

Waziri Ummy ameeleza kuwa aliyefariki ni mwanaume mwenye umri wa miaka 49 ambaye alikuwa katika kituo cha kuhudumia wagonjwa wenye virusi vya Corona cha Mloganzila jijini Dar es salaam na kuwa licha ya virusi vya Corona marehemu alikuwa akisumbuliwa na maradhi mengine.

Kifo hicho kimetokea wakati Tanzania ikiwa na jumla ya wagonjwa 19 wa virusi vya Corona na kati ya hao mmoja amepona na mmoja amefariki dunia.

March 31, 2020

Tanzania Kutowaumiza wanachi katika Tahadhari dhidi ya Corona
Tanzania Kutowaumiza wanachi katika Tahadhari dhidi ya Corona

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amesema kuwa kama nchi haiwezi kuchukua tahadhari kama zilivyochukuliwa na Mataifa mengine duniani ya kupambana na Virusi vya Corona kwa kuwa watu wengi nchini maisha yao ni ya kubangaiza siku kwa siku.

Hayo ameyabainisha Machi 31, 2020, Jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa Bunge la 11 Mkutano wa 19 ambapo ametoa nafasi ya wabunge waliohudhuria kutoa maoni juu ya kupambana na ugonjwa huo.

"Hatuwezi kuchukua measure za wazungu na kuzi copy na ku- paste hapa kwetu kama zilivyo, tutaua watu wetu, lazima tuangalie maisha yetu ya Kitanzania na kujaribu kuchukua hatua kufuatana na mazingira yetu" amesema Spika Ndugai.

Wakati huo Mbunge wa jimbo la Kawe jijini Dar Es Salaam Mhe.Halima Mdee ameishauri Serikali kufanya mchakato wa kupima Corona wabunge wote na watakaobainika wawekwe karantini ili watakaokuwa salama waweze kushiriki vikao vya bunge kwa pamoja.

March 31, 2020

CAG abaini madudu vyama vya siasa CCM na CUF katika ukaguzi wake
CAG abaini madudu vyama vya siasa CCM na CUF katika ukaguzi wake

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere amebainisha mapungufu katika ukaguzi wake kwenye vyama vya siasa vya CUF na CCM.

Kichere amebainisha hayo Alhamisi Machi 26 katika Ikulu jijini Dodoma wakati akiwasilisha ripoti ya ukaguzi wake ya 2018/19 kwa Rais John Magufuli ambapo katika ukaguzi wake alibaini chama cha wananchi CUF kilipokea ruzuku ya Sh369.38 milioni lakini kiasi cha Sh300 milioni kilihamishwa kutoka kwenye akaunti ya chama kwenda kwenye akaunti binafsi.

Pia, amesema chama hicho kimeondoa saini ya katibu mkuu kama mmoja wa watu wa kuidhinisha utoaji wa fedha kutoka kwenye akaunti ya chama.

Kwa upande wa Chama cha mapinduzi CCM, Kichere amesema Jumuiya ya Wazazi ilimuondoa mpangaji wake bila kufuata utaratibu, jambo lililosababisha mpangaji kutishia kufungua kesi akitaka kulipwa fidia ya Sh800 milioni.

Hata hivyo, amesema jumuiya hiyo ilimlipa Sh60 milioni baada ya kufanya mazungumzo ya kirafiki na mpangaji huyo ili kumaliza mgogoro uliokuwepo.

March 26, 2020

Iadadi ya Wagonjwa wa Corona wafikia 13 nchini Tanzania
Iadadi ya Wagonjwa wa Corona wafikia 13 nchini Tanzania

Waziri wa Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto nchini Tanzania Ummy Mwalimu, amesema idadi ya wagonjwa wa corona imefikia 13 ambapo kati yao 8 ni Watanzania na watano ni wageni

Waziri Ummy ameyabainisha hayo leo Machi 26, 2020, wakati akitoa taarifa kwa umma, kuhusu hali ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini

Amesema kati ya wagonjwa hao Dar es Salaam wapo nane, Arusha wawili, Zanzibar wawili na Kagera mmoja.

Waziri Ummy amesema kuwa mgonjwa wa 13 alipatikana mkoani Kagera na ni dereva wa magari makubwa, ambaye aliingia nchini kupitia mpaka wa Kabanga na shughuli zake anafanyia kati ya Burundi, DRC na Tanzania.

Pia amesema mgonjwa wa kwanza nchini wa virusi vya corona, Isabela Mwampamba (46) ameshapona ugonjwa huo.

“Mgonjwa wetu wa kwanza ambaye haturuhusiwi kutaja jina lakini alijitaja mwenyewe amepona COVID 19, tumepima sampuli mara tatu na zote zimeonyesha negative, tumeanza utaratibu wa kumruhusu kurudi nyumbani,” amesema.

March 26, 2020

Rais Magufuli Asema Corona haizuii Uchaguzi mkuu 2020,
Rais Magufuli Asema Corona haizuii Uchaguzi mkuu 2020

Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amesema Ugonjwa wa Corona hautaizuia Tanzania kufanya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Rais Magufuli amesema uchaguzi utafanyika kama ilivyopangwa na kuwa mripuko wa ugonjwa wa mafua makali unaosababishwa na kirusi cha Corona hauwezi kuwa sababu ya kusitisha uchaguzi nakuwa hakuna Mtu anayependa kukaa Ofisini muda mrefu.

Suala la uchaguzi limehutubiwa wakati Rais huyo akipokea taarifa ya ukaguzi kutoka kwa mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali CAG, na taarifa ya Taasisi ya kuzuia na kupmbana na rushwa TAKUKURU Ikulu jijini Dodoma.

March 26, 2020

Tanzania Yaunda kamati kuzuia kusambaa virusi vya Corona
Tanzania Yaunda kamati kuzuia kusambaa virusi vya Corona

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania inaendelea kufanya tathmini ili kuhakikisha inazuia ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) isiweze kusambaa nchini.

Majaliwa amevishukuru vyombo vya habari nchini kwa ushirikiano wanaoutoa kwa Serikali katika kuelimisha umma namna ya kujikinga na virusi vya corona.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo Jumatatu, Machi 23, 2020 wakati akizungumza na Mawaziri na Makati Wakuu katika Kikao Kazi kilichofanyika jijini Dodoma.

Imeelezwa kuwa kinga dhidi ya virusi vya corona liwe ni jambo la kimkakati zaidi kuliko kusubiri kutibu, hivyo kwa sasa Serikali imeweka mkazo kwenye kuwahamasisha wananchi kujikinga na virusi hivyo.

Akizungumzia kwa upande wa Tanzania, Waziri wa afya maeneleo ya jamii jinsia wazee na watotoUmmy Mwalimu amesema jumla ya watu 12 walibainika kuwa na virusi vya corona tangu mgonjwa wa kwanza alivyogundulika nchini na kwamba wagonjwa wote hali zao ni nzuri na mmoja amepimwa zaidi ya mara mbili na kubainika kuwa hana virusi tena.

March 24, 2020

ATCL yafuta safari zake nchini Comoro
ATCL yafuta safari zake nchini Comoro

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imefuta safari zake za kwenda nchini Comoro, na hivyo kuifanya iwe imefuta safari zake kwenda kwenye mataifa manne tangu kutokea kwa mlipuko wa virusi vya corona duniani.

Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi amesema kuwa ndege ya ATCL inafanya safari yake ya mwisho kutoka Dar es salaam kwenda Comoro, na baada ya hapo abiria ambao tayari wamekata tiketi kwa ajili ya safari watarudishiwa fedha zao bila chaji yoyote ya ziada.

Safari nyingine zilizofutwa na ATCL kwenda nje ya nchi ni pamoja na kwenda Mumbai nchini India baada ya serikali ya nchi hiyo kuzuia wageni kuingia nchini humo hadi Aprili 15 mwaka huu, ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Safari nyingine zilizofutwa na ATCL ni ile ya kutoka Dar es salaam kwenda Entebbe Uganda na kutoka Dar es salaam kwenda Bujumbura Burundi.

March 24, 2020

CHADEMA yasitisha mikutano kisa Corona
CHADEMA yasitisha mikutano kisa Corona

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesitisha tamko lake la kufanya mikutano ya hadhara kote nchini kutokana na ugonjwa wa Corona

Mikutano hiyo iliyotangazwa kufanyika kuanzia April 04 mwaka huu imesitishwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Mh.Freeman Mbowe jijini Dodoma.

Akizungumza leo Machi 23, 2020, Jijini Dodoma, Mbowe amesema kuwa wakati anatoa kauli yake ya kutangaza uwepo wa mikutano ya hadhara kwa nchi nzima, Serikali haikuwa imetangaza uwepo wa mgonjwa yeyote wa Virusi vya Corona na kwamba wataendelea na mikutano yao pale ambapo hali ya ugonjwa huo itakuwa imetengemaa.

Aidha Mbowe ameiomba Serikali kuchukua hatua ya kufunga mipaka yake yote ili kuhakikisha hakuna mgeni yoyote anayeingia nchini kutoka kwenye Mataifa yaliyoathirika na Virusi vya Corona.

March 24, 2020

Rais Magufuli Awasimamisha Wahandisi 12 TANROADS
Rais Magufuli Awasimamisha Wahandisi 12 TANROADS

Rais magufuli amewasimamisha Kazi Wahandisi 12 Waliopo Ofisi Ya Tanroads Mkoani Morogoro Akiwemo Kaimu Meneja Aliyehamishiwa Makao Makuu Kwa Agizo La Waziri Mkuu Na Kuwapa Onyo Kali Na La Mwisho Viongozi Wa Juu Wa Wizara Ya Ujenzi Uchukuzi Na Mawasiliano Pamoja Na Wakala Wa Barabara.

Rais magufuli amefikia uamzi huo wakati alipotembelea na kukagua daraja la Mkange Kegeya Kwa Mara Ya Kwanza Na Kujionea Yaliyojiri huku pia akionesha kutoridhishwa na matukio ya kukatika kwa madaraja na barabara.

Katika ziara hiyo akiwa jijini Dar es salaam Rais Magufuli ametumia fursa hiyo kutangaza kufuta mbio za Mwenge mwaka 2020 hadi pale ugonjwa wa corona utakapoisha.

Amesema fedha za mwenge ambao ulitakiwa kuwashwa Zanzibar zitatumika katika kujiandaa na tahadhari dhidi ya corona.

March 20, 2020

Tanzania yathibitisha Mgonjwa Wa Corona
Tanzania yathibitisha Mgonjwa Wa Corona

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amethibitisha kuwa Tanzania ina mgonjwa mmoja mwanamke (46) mwenye virusi vya Corona, aliyeingia nchini kwa ndege ya Rwandair kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akitokea nchini Ubelgiji.

Waziri huyo ametoa taarifa hiyo Jumatatu Machi 16, 2020, alipokutana na waandishi wa habari katika ofisi za Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Tafiti za Tiba (NIMRI).

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na wizara yake, mgonjwa huyo ambaye alipita katika nchi za Sweden, Denmark na Ubelgiji kabla ya kurejea nchini, alipelekwa katika kituo maalum cha kuwahifadhi na kuwahudumia waathirika wa Corona kilichopo nje kidogo ya Hospitali ya Mawenzi mkoani Kilimanjaro ambapo anapatiwa matibabu na anaendelea vizuri.

“Nimeongea naye mgonjwa huyo leo tena mara kadhaa, anazungumza vizuri tu, lakini katika maelezo yake anasema alikuwa Ubelgiji, kwenye nyumba aliyofikia, mume wa mwenyeji wake alikutwa na maambuziki ya ugonjwa wa Corona.

Aidha, amesema serikali inawafuatilia watu wote aliokutana nao mgonjwa huyo ili kuwaweka katika chumba maalum kwa ajili ya uangalizi kwa siku 14.

March 20, 2020

CHADEMA yatangaza kufanya mikutano ya hadhara
CHADEMA yatangaza kufanya mikutano ya hadhara

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema kuwa kuanzia Aprili 4, 2020, chama hicho kitaanza rasmi kufanya mikutano ya hadhara yenye malengo mawili kudai tume huru na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu.

Akizungumza na wana habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, alisema lengo pia ni kufanya maandalizi ya uchaguzi mkuu mwaka huu.

Mbowe aliwatangazia viongozi wote wa Chadema katika mikoa na wilaya kuanza kufanya mikutano hiyo licha ya kupigwa marufuku na serikali tangu mwaka 2016 na kwamba hawatahitaji kibali kufanya mikutano hio kwa kile alichodai ni haki yao ya kikatiba.

“Kuanzia Aprili 4, mwaka huu hatutasubiri kibali cha mtu yeyote tutaanza mikutano nchi nzima na kwa kauli hii na watangazia viongozi wote wa Chadema tuanze kufanya mikutano ya hadhara tukidai vitu viwili tume huru ya uchaguzi na maandalizi ya uchaguzi,” alisema Mbowe.

Alisema hatua yake ya kwenda Mwanza katika maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania Bara, ambazo mgeni rasmi alikuwa Rais John Magufuli, lengo lake lilikuwa kufanyika kwa maridhiano ya kitaifa kati ya vyama na wadau wengine wa siasa, na ndio sababu ya kumwandikia barua ya kuomba kukutana nae, lakini ameshangazwa na kutokujibiwa kwa barua yao hadi sasa.

March 20, 2020

Siku kumi wakandarasi REA kutoa ripoti kwa ma RC na DC
Siku kumi wakandarasi REA kutoa ripoti kwa ma RC na DC

Wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa kusambazaji Umeme Vijijini(REA) wameagizwa kutoa orodha ya vijiji wanavyosambaziwa umeme kwa Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa ndani ya mwezi huu ili viongozi hao watoe majibu ya uhakika kwa wananchi.

Hayo yamebainisha na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma.

Dkt.Kalemani amesema kuwa kila mkandarasi anatakiwa kuwasilisha mpango kazi wa kufikisha umeme maeneo ambayo bado hayajafikiwa kwa viongozi hao ndani ya mwezi huu ili watoe majibu kwa wananchi pindi watakapotaka kujua lini watapatiwa umeme maeneo yao.

“Hili litasaidia viongozi hao kuwapatia majibu sahihi wananchi wao wanao waongoza iwapo yatatokea maswali ya kutaka kufahamu ni lini watafikiwa katika kupatiwa umeme”amesema Dkt. Kalemani

Aidha, Dkt.Kalemani amesema kuwa nguzo ambazo zimewekwa chini katika maeneo yao ya kazi zisimamishwe sambamba na kufunga transfoma na kukaza nyaya zilizolala ndani ya mwezi huu zoezi hilo liwe limekamilika

March 20, 2020

NECTA yasitisha mitihani kidato cha sita na vyuo
NECTA yasitisha mitihani kidato cha sita na vyuo

Baraza la Mitihani nchini (Necta) limetangaza kuahirisha mitihani ya kidato cha sita na ualimu iliyokuwa ifanyike Mei 4 mwaka huu 2020 hadi pale itakapotoa taarifa mpya.

Hatua hiyo imekuja baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Machi 17, kutangaza kufungwa shule na vyuo vyote ili kuondoa misongamano na kupambana na virusi vya ugonjwa wa corona.

Kupitia maagizo hayo Necta imetoa maelekezo kwa maofisa elimu wa wilaya kuwajulisha wakuu wa shule na vyuo vya ualimu nchini wawajulishe watahiniwa kuhusu kuahirishwa kwa mitihani hiyo.

Mpaka sasa hakuna taasisi yoyote ya kielimu nchini Tanzania inayoendelea kutoa mafunzo ikiwa ni kuanzia shule za awali mpaka vyuo vikuu na shughuli hizo zikisitishwa kwa muda wa mwezi mmoja.

March 20, 2020

Shughuli za Bunge Tanzania kuendeshwa kwa mtandao
Shughuli za Bunge Tanzania kuendeshwa kwa mtandao

Bunge la Tanzania limesitisha utaratibu wa kupokea wageni mbalimbali wakiwamo wanafunzi wanaokwenda bungeni kwa lengo la kuona na kujifunza shughuli za Bunge.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Machi 19, 2020 na kitengo cha mawasiliano na uhusiano wa kimataifa cha ofisi ya Bunge imesema hatua hiyo ni mikakati ya muhimili huo uliotangazwa na Spika Job Ndugai wa kujinga na maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Taarifa hiyo imesema wageni watakaoruhusiwa kuingia bungeni ni wale wenye kazi na vibali maalum tu.

Katika taarifa yake spika Ndughai kwa waandishi wa habari inaeleza kuwa vikao vya kamati zote za bunge vitaendeshwa kwa njia ya mtandao katika kuelekea vikao vya bunge vinavyotarajiwa kuanza machi 31 mwaka huu.

March 20, 2020

Tabora mkoa unaoshiriki kutokomeza malaria Tanzania
Tabora mkoa unaoshiriki kutokomeza malaria Tanzania

Mkoa wa Tabora umezindua kampeni ya kutokomeza malaria inayofahamika kama ziro malaria inaanza na mimi ambapo taarifa zinaonesha bado maambukizi ya ugonjwa huo katika mkoa wa Tabora bado yako juu ambapo katika ngazi za wilaya halmashauri ya Kaliua inaongoza katika maambukizi ya malaria.

Akitoa taarifa juu ya maambukizi ya ugonjwa wa malaria mkoa wa Tabora mganga mkuu wa mkoa Dkt Honoratha Rutatinisibwa amesema kwa kipindi cha miaka itatu taarifa zinaonesha kupungua maambukizi hayo huku katika ngazi za wilaya halmashauri ya wilaya ya Kaliua ikionesha kiwango cha juu kwa aslimia 16 ya maambukizi ya malaria ikiwa zaidi ya halmashauri zote.

Dkt. Honoratha amewatowa wasiwasi wananchi juu uvumi wa kuwa matumizi ya vyandarua vyenye dawa husababisha magonjwa.

Kutokana na kusambaa uvumi unaoeleza kuwa utumiaji wa vyandarua vyenye dawa kuna madhara katika afya ya binadamu nakupelekea matumizi ya vyandarua kuwa nje ya matarajio serikali ya mkoa kupitia kwa mkuu wake wa mkoa Aggrey Mwanri ameagiza kukamatwa kwa wale wote watakaokutwa wakitumia vyandarua mashambani na kufugia kuku.

March 09, 2020

Jamii Tanzania yaanza vita dhidi ya ukatili kwa wanawake na watoto
Jamii Tanzania yaanza vita dhidi ya ukatili kwa wanawake na watoto

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekemea vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto hasa wakiume ambao wamekuwa wakidhalilishwa kwa kuwaingilia kinyume na maumbile.

Ameyasema hayo mkoani Simiyu wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kitaifa mkoani Simiyu.

Samia Amewataka watanzania kusimama pamoja na kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzie katika mapambano ya kuondokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Amezitaka Kamati za ulinzi wa Wanawake na watoto kufanya kazi na kuacha kujuana ili Sheria ichukue mkondo wake pale inapotokea mtu amefanya kitendo cha kikatili.

Naye Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa agenda ya usawa wa kijinsia sio ya wanawake peke yao ila ni kwa wote yani wanawake na wanaume ili kuweza kuleta usawa wa kijinsia.

March 09, 2020

Diwani auawa kwa kukatwa mapanga Tabora
 Diwani auawa kwa kukatwa mapanga Tabora

Diwani kata ya Usunga wilayani Sikonge mkoa wa Tabora ameuawa kwa kuvamiwa na watu wasiojulikana usiku nyumbani kwake kwa wakimjeruhi kwa kutumia vitu vyenye ncha kali vikidhaaniwa kuwa ni panga.

Diwani huyo aliyefahamika kwa jina la Alfred Masamalo amefariki march 4 akiwa na umri wa miaka 47 ameacha mke na watoto sita (6).

Akitoa taarifa juu ya wahusika wa tukio hilo kamishna msaidizi wa polis mkoa wa Tabora Laurian Fabian amesema kuwa mpaka kufikia march 7 watu 6 wanaoshukiwa kuhusika na tukio hilo tayari wanashikiliwa na jeshi la polisi nakuwa msako mkali unaendelea ili kumbaini mhusika.

Katika ibaada ya kuaga mwili wa marehemu, mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amesema wananchi wasiingilie kwa aina yoyote juu ya maamzi ya vyombo vya ulinzi na usalama katika kumsaka mhusika wa tukio hilo nakuwa lengo nikuhakikisha mauaji katika mkoa wa Tabora yanatokomezwa.

Matukio ya kuuawa kwa madiwani yamekuwa yakiripotowa ambapo madiwani wawili katika halmashauri ya wilaya ya uyui wakiwa katika nafasi ya mwenyekiti wa halmashauri waliuawa,na diwani mmoja katika wilaya ya Urambo naye akiripotiwa kuuawa na watu wasiojulikana' Taarifa iliyotolewa na mkuu wa mkoa Aggrey Mwanri.

March 09, 2020

Mahakama yakubali maombi ya Rugemalila
Mahakama yakubali maombi ya Rugemalila

Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu imekubali kupokea hoja za maombi ya mfanyabiashara James Rugemalira anayetaka kuondolewa kwenye kesi ya utakatishaji fedha wa Sh. Bil 309.4.

Wakili wa utetezi, John Chuma amedai kuwa mteja wake ameshawasilisha hoja za pingamizi la awali lakini hajapata majibu yoyote kutoka upande wa Jamuhuri.

Akijibu hoja hizo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai baadhi ya nyaraka amezipata mahakamani hapo na kuwa upande wa Jamhuri upo tayari kusikiliza hoja hizo kwa njia ya mdomo.

Baada ya hoja hizo, Hakimu Shaidi Shaidi ameahirisha shauri hilo hadi Machi 12, 2020 litakapokuja kwa ajili ya kutajwa na upande wa jamuhuri kuwasilisha majibu.

February 28, 2020

COMESA SADC NA EAC kuing’arisha Tanzania
COMESA SADC NA EAC kuing’arisha Tanzania

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe amepokea ujumbe kutoka Sekretarieti ya Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) ulioongozwa na Balozi Dr.Kipyego Cheluget, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia miradi.

Ujumbe huo umefika katika ofisi za wizara zilizopo katika eneo la Mtumba jijini Dodoma lengo likiwa ni kukutana na Menejimenti ya Wizara kuzungumzia utekelezaji wa mradi unaohusu uwezeshaji biashara na kuimarisha biashara ya mipakani (Cross Border Trade).

Pande zote mbili zimekubaliana kushirikiana kwa karibu zaidi katika utekelezaji wa mradi huo ambao unatarajia kuchochea na kurahisisha biashara kwa nchi wanachama wa Jumuiya za COMESA, EAC na SADC.

February 28, 2020

Tabora mjini uhaba wa maji imebaki ndoto.
Tabora mjini uhaba wa maji imebaki ndoto.

Maji Kutoka Ziwa Victoria Yameingia Mjini Tabora Kwenye Tank La Itumba Lenye Ujazo Wa Lita Elf 9 Ikiwa Ni Sehemu Ya Utekelezaji Wa Mradi Huo Mkubwa Wa Maji Unaogharimu Zaidi Ya Bil 600.

Mradi huo Unalenga Kuondoa Adha Ya Maji Katika Mkoa Wa Tabora Kwa Kuwanufaisha Wananchi Mil 1.2 Hadi Ifikapo Mwaka 2035

Mhandisi William Kazenga Ambaye Ni Mkurugenzi Msaidizi Matengenezo Idara Ya Maji Akiwa Ameambatana Na Wataalam Wengine Wameweka Kambi Katika Eneo La Tank Hilo Huku Akiwahakikishia Wananchi Kuwa Muda mfupi Wataanza Kutumia Maji Hayo Majumbani

Maji hayo Tayari yameshajazwa katika Matenki ya Wilaya Za Nzega,Igunga,Uyui Na Sasa Tabora Mjini Ikiwa Ni Hatua Za Mwisho Kabisa Za Ukamilishaji Wa Mradi Huo.

February 28, 2020

Serikali Kuchukua kiwanda kilichobinafsishwa
Serikali Kuchukua kiwanda kilichobinafsishwa

Kamati kuu ya ya siasa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Tabora imeridhia kurejeshwa serikalini kiwanda cha nyuzi Tabora baada ya mwekezaji kushindwa kukiendesha.

Mapendekezo hayo yamefikiwa wakati wa uwasilishaji taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM ambapo katika sekta ya uchumi na uwekezaji katika kiwanda cha nyuzi Tabora taarifa imeonyesha kushindwa kwa mwekezaji tangu kuanza kwake mwaka 2004.

Agizo hilo limewasilishwa na mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri likiridhiwa na katibu tawala msaidizi uchumi na uwekezaji Bw Raphael Nyanda.

Wakati huo mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Tabora Bw:Hassan Wakasuvi amewatadharisha wagombea kupitia chama hicho kuwa wakishindwa katika matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu wasikate tamaa kufuatia kuwa uchaguzi ni wakidemokrasia.

February 21, 2020

IGP Sirro, magaidi hawana nafasi
IGP Sirro, magaidi hawana nafasi

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amefungua na kuongoza mkutano wa Kamati Tendaji za Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki mwa Afrika (EAPCCO).

Kamanda Sirro amesema kwa Tanzania mtu yeyote mwenye nia ya kuanzaisha vitendo vya kigaidi hatapata nafasi hiyo kutokana kuwa nchi hiyo haina tamaduni hizo.

Amesema iwapo mtu atajiingiza katika mipango hiyo kutoka kwake ni ngumu huku akitumia msemo usemao kuwa “ukiua kwa upanga utauawa kwa upanga”

Mkutano huo umeshirikisha nchi 14 kutoka kwenye shirikisho hilo ambapo wamekutana kujadili na kupanga mikakati ya kupambana na uhalifu unaovuka mipaka.

February 21, 2020

Rais Magufuli ,Tanzania Tunaimarisha sekta ya Afya
Rais Magufuli ,Tanzania Tunaimarisha sekta ya Afya

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema katika kipindi cha miaka minne ya utawala wake, Serikali imeweza kuajiri watumishi wapya 13479 wa sekta ya afya sambamba na kuimarisha na kuboresha miundombinu ya huduma za afya za ikiwemo ujenzi na ukarabati wa zahanati, vituo vya afya na hospitali za wilaya katika maeneo mbalimbali nchini.

Katika maadhimisho ya siku ya madaktari alhamis 20, Amesema kuwa Serikali ya Awamu yake imeendelea kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma za afya nchini ikiwemo kuongeza idadi ya rasilimali watu, ambapo hadi kufikia Julai 2019, jumla ya watumishi wa kada ya afya 98987 walikuwa tayari wamekwishajiriwa wakiwemo 18904 waliopo katika sekta binafsi.

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dkt. Elisha Osati ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kutokana na mageuzi mbalimbali iliyoyafanya na inayoendelea kufanya katika kuboresha huduma za matibabu kwa wananchi na taasisi hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi na mipango mbalimbali ya Serikali.

February 21, 2020

Waziri Lukuvi amfukuza kazi ofisa ardhi
Waziri Lukuvi amfukuza kazi ofisa ardhi

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , William Lukuvi amemsimamisha kazi ofisa ardhi wa Wilaya ya Kigamboni ambaye siku kadhaa zilizopita Rais Magufuli alitaka achukuliwe hatua kwa kile alichoeleza kuwa ni mtoro

Katika maelezo ya Lukuvi ya february 16 wakati akikabidhi ekari 715 za ardhi kwa manispaa ya Kigamboni amesema kama alivyoagizwa na Rais Magufuli, anamsimamisha kazi mtumishi huyo.

Waziri lukuvi amesema walishapata barua kutoka kwa mkurugenzi wa Kigamboni hivyo wanamsimamisha wakati hatua za kinidhamu zikiendelea na Kama kutakuwa na uhitaji wataleta mtu mwingine.

February 18, 2020

RC Mwanri, Makanisa hubirini amani
RC Mwanri, Makanisa hubirini amani

Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amelitaka kanisa kuwa mstari wa mbele katika kuhubiri amani taifa linapoelekea katika uchaguzi mkuu

Mwanri amehudhuria ibada ya umoja wa makanisa (CCT) mkoa wa Tabora iliyofanyika jumapili ya February 16, amesema katika sheria ya Tanzania serikali imewapa watu uhuru wa kuabudu huku akigusia amani ya nchi hasa kuelekea katika uchaguzi mkuu

Baadhi ya waumi waliohudhuria ibada hiyo wamesema imekuwa ibada ya Baraka, wamemuona mungu akiwatumia watumishi wake.

February 18, 2020

Rais Magufuli abaini upigaji TASAF
Rais Magufuli abaini upigaji TASAF

Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli hapo jana Amezindua Kipindi Cha Pili Cha Awamu Ya Tatu Ya Utekelezaji Wa Mpango Wa Kunusuru Kaya Maskini Kupitia Mfuko Wa Maendeleo Ya Jamii TASAF.

Rais Magufuli Amesema Katika Utekelezaji Wa Mpango Huo Wa Tasaf Zimejitokeza Changamoto za Uhakiki Wa Kaya Maskini Uliofanyika Kuanzia Novemba 2015 Hadi Juni 2017 Zilithibitika Kaya Hewa Sabini Na Tatu Elfu Na Mia Tano Sitini Na Moja Pamoja Na Kaya Ishirini Na Mbili Elfu Thelathini Na Nne Zilithibitika Sio Maskini

Amesema Hali ya umaskini wa kipato hapa nchini Mwaka 1991-92 ulikuwa Asilimia 39, 2007 umaskini ulikuwa asilimia 34, 2012 Asilimia 28.4 na 2018 hali ya umaskini likuwa 26.4, na kwamba kasi ya kupunguza umaskini hapa nchini inaenda kwa kasi.

February 18, 2020

Tanzania mwenyeji kamati ya maafa SADC
Tanzania mwenyeji kamati ya maafa SADC

Serikali ya Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kwanza wa Kamati ya Mawaziri wenye dhamana ya Menejimenti ya Maafa kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika utakaofanyika tarehe 18 – 21 Februari, 2020, Zanzibar.

Mgeni Rasmi, atakayefungua mkutano huo ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ally Mohamed Shein

Kaulimbiu ya Mkutano huu ikiwa ni Ushiriki wa Kisekta kwenye Kupunguza madhara ya maafa ni njia bora ya kuimarisha ustahimilivu katika ukanda wa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika” (SADC

Mkutano huu unafanyika kwa mara ya kwanza visiwani Zanzibar tangu Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akabidhiwe uenyekiti wa jumuiya.

February 14, 2020

Serikali kumhoji aliyetangaza kutibu Corona.
Serikali kumhoji aliyetangaza kutibu Corona.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewahakikisha Watanzania kuwa nchi iko salama na hakuna mgonjwa yeyote mwenye Virusi vya Corona.

Amesema kuwa Serikali imekuwa ikifuatilia taarifa mbalimbali za washukiwa na watu wote ambao tunawahisi kuwa na ugonjwa huo na tumeweza kuwapima na kubaini kuwa hawana ugonjwa.

Akijibu kuhusu mtu ambaye anasema kuwa anayo dawa ya kutibu ugonjwa huo ambaye anajulikana kwa jina la Mosses Mollel maarufu “Nabii namba saba” Dkt Ndugulile amesema kuwa anazo taarifa za mtu huyo na kumtaka athibitishe kauli yake.

February 14, 2020

Wauzaji wa maziwa kuchochea magonjwa
Wauzaji wa maziwa kuchochea magonjwa

Imeelezwa kuwa wauzaji wengi wa maziwa hawazingatii taratibu za afya kwani huchanganya maji kwenye maziwa jambo ambalo linamadhara makubwa kwa afya ya mtumiaji.

Pascal Matage ambaye ni afisa afya manispaa ya Tabora amesema yapo madhara iwapo mtu atatumia maziwa yaliyochanganywa na maji ikiwa ni pamoja na kukosa virutubisho halisi, sambamba na kupata magonjwa yatokanayo na maji hayo yasiyo salama.

Hata hivyo Matage amesisitiza utumiaji wa maziwa kwa wingi ili kuimarisha afya ambapo mtu mmoja kwa mwaka mzima anapaswa kutumia lita 200 za maziwa.

Kufuatia kauli hiyo ya afisa afya manispaa ya tabora redio uhai imepata nafasi ya kuzungumza na wananchi ili kufahamu ikiwa wana uelewa kuhusiana na suala hilo na wamesema hawana uelewa wowote huku wakikiri kupata madhara ya kuhara pindi wanapotumia maziwa wasiyojua usalama wake.

February 14, 2020

Zitto Kabwe ashindwa kufika mahakamani
Zitto Kabwe ashindwa kufika mahakamani

SERIKALI ya Tanzania kupitia Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imefanikiwa kupata amri za kutaifisha mali na fedha zinazohusiana na uhalifu sambamba na fedha zilizolipwa kutokana na kesi za madini zilizopo katika akaunti ya AFR katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zenye thamani ya Tsh Bilioni 58.6.

Kwa upande wake Waziri wa Madini, Dotto Biteko aliwataka wachimbaji na wafanyabiashara wa madini nchini kuzingatia sheria kwa kuwa serikali haitokuwa na msamaha kwa mtu yoyote atakayejihusisha na vitendo vya utoroshaji wa rasimali madini nje ya nchi kwani yamechangia kwa kiasi kikubwa katika kuinyima nchi mapato.

Aidha Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango alisema zoezi la utaifishaji wa mali za uhalifu, ni dalili tosha kuwa Tanzania sio nchi maskini na hivyo hakuna sababu ya Serikali kwenda kukopa nje ya nchi na badala yake itaendelea kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha kuwa raslimali zake zitalindwa kwa nguvu zote.

February 11, 2020

Zitto Kabwe ashindwa kufika mahakamani
Zitto Kabwe ashindwa kufika mahakamani

Mdhamini wa Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe ameileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mbunge huyo ameshindwa kufika mahakamani hapo jana baada ya kuugua akiwa nje ya nchi.

Ray Kimbita ameeleza hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutolewa uamuzi kama ana kesi ya kujibu au la baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi.

Hata hivyo Wakili wa Serikali mwandamizi, Nassoro Katuga amedai kuwa mshtakiwa anapokuwa nje ya nchi ni jukumu la mdhamini kujua alipo kwani Kitendo cha mdhamini huyo kupigiwa simu na mtu mwingine ina maana hajawasiliana na mshtakiwa na hajui alipo, atakaporudi aieleze Mahakama sababu za kutowasiliana na mdhamini wake pamoja na udhibitisho wa kuugua,”

Baada ya kueleza hayo Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 18, mwaka huu na kumtaka mdhamini huyo kujitathimini kwa kuwa ameshindwa kujua mshtakiwa alipo.

February 11, 2020

Rais Magufuli kuizindua wilaya ya Kigamboni
Rais Magufuli kuizindua wilaya ya Kigamboni

Rais Magufuli leo anatarajiwa Kuzindua Rasmi Wilaya Mpya ya Kigamboni ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa Wingi katika Uzinduzi huo wa Kihistoria.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amesema hafla ya Uzinduzi huo inaanza asubuhi ya leo kwenye Viwanja vya Mkuu wa Wilaya ambapo Rais Magufuli atazindua Jengo la Utawala la Mkuu wa Wilaya, Jengo la Halmashauri na Majengo ya Hospital ya Wilaya ya Kigamboni.

Uzinduzi huo unakuja wakati muafaka ambao Tayari Serikali imefanya juhudi kubwa za Maendeleo katika Wilaya hiyo kupitia Miradi mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa Barabara za Lami, Ujenzi wa Hospital, Vituo vya Afya, Zahanati, Huduma za maji, Elimu pamoja na huduma zote muhimu.

February 11, 2020

Wanawake kuutangaza utalii Tanzania
Wanawake kuutangaza utalii Tanzania

Chama cha wanawake sekta ya utalii Tanzania AWOTTA kimetetakiwa kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa utalii wa ndani.

Wito huo umetolewa jijini dar es salaam na mkurugenzi wa bodi ya utalii Tanzania Bi. Devotha Mdachi wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya pili ya utalii wa ndani yaliyoandaliwa na chama cha wanawake sekta ya utalii nchini.

Amesema wananchi ndiyo wanaokuza mapato ya nchi kupitia utalii.

Bi. Mdachi amesema chama hicho ni chachu ya kuwahamasisha wanawake kutumia fursa ya utalii ili kufikia mafanikio ya kuitangaza Tanzania na kukuza mapato kupitia utalii wa ndani.

February 7, 2020

TCRA yatahadharisha wanahabari kuhusu uchaguzi
TCRA yatahadharisha wanahabari kuhusu uchaguzi

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA) kanda ya kati ikijumuisha mkoa wa Tabora na Kigoma imetoa semina ya kuwajengea uwezo wandishi wa habari namna ya kuaandaa taarifa za uchaguzi.

JOSEPH MAPUNDA makamu mwenyekiti kamati ya maudhui ya TCRA kanda ya kati amesema kuwa vyombo vya habari ni nyenzo ya kujenga misingi ya kuheshimiana bila kuweka uchochezi.

Aidha MAPUNDA amewataka wananchi pindi uchaguzi utakapofika kuwa makini katika kuchagua kiongozi ambaye anafaa bila kujali ushabiki wa chama na kutotumia vibaya mitandao hali inayoweza kupelekea kufungwa na sheria.

February 7, 2020

Rais asema upelelezi wa kesi uharakishwe
Rais asema upelelezi wa kesi uharakishwe

Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ametaka upelelezi wa kesi za watu mbalimbali kufanyika kwa haraka.

Rais magufuli ametoa wito huo jijin dar es salaa wakati wa maadhimisho ya wiki ya sheria nchini ambapo amewataka wapelelezi kote nchini kuhakikisha wanaharakisha mchakato wa uchunguzi pale mtu anapokamatwa ili kupunguza mrundikano wa kesi katika mahakama

Rais magufuli amesema ni jukumu la kila mtu wakiwemo watumishi wa umma kufunga mkanda na ku toweke maslahi binafsi mbele ikiwemo kutaka kuongezewa mishahara kwani sasa taifa linafanya uwekezaji mkubwa kwa kizazi kijacho.

February 7, 2020

Rais Magufuli awaapisha viongozi wateule.
Rais Magufuli awaapisha viongozi wateule.

Rais wa jamuhuri wa muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha viongozi mbali mbali aliowachagua mwishoni mwa wiki iliyopita na kuwataka viongozi hao kushirikiana vyema katika utendaji wao wa kazi.

Miongoni mwa walioapishwa na Rais Magufuli ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbasi, Katibu Mkuu wizara ya Nishati, Bi Zena Ahmed Said, katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Riziki Shemdoe, Katibu Mkuu wizara ya mambo ya ndani ya Nchi Christopher Kadilo, Katibu Mkuu wizara ya Ardhi Bi Marry Gaspar Makondo.

Hafla ya kuwaapisha viongozi hao imeafanyika ikulu jijii dar es salaam.

February 4, 2020

Millioni 19 Kuinua sekta ya Afya Tabora
Millioni 19 Kuinua sekta ya Afya Tabora

Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amepokea vifaa vya ujenzi pamoja na vifaa vya hospitalini vyenye thamani zaidi ya shilingi million 19 kutoka kampuni ya alliance one ambavyo vitagawiwa katika baadhi ya halmashauri kwa ajili ya kusaidia sekta ya afya.

Akikabidhi vifaa hivyo mkurugenzi wa uzalishaji kampuni ya alliance one Bw David Mayunga amesema wametoa vifaa hivyo kutokana na kuwa wadau wakubwa katika jamii ya mkoa wa Tabora nakuwa kampuni hiyo inalenga kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na maisha bora.

Baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo Mkuu wa mkoa Aggrey Mwanri amemtaka mganga mkuu wa mkoa kuvitunza kwa umakini huku akitaka vifaa hivyo vitumike katika matumizi yaliyokusudiwa.

February 4, 2020

Mabilioni ya pesa kuboresha kilimo cha Pamba
Mabilioni ya pesa kuboresha kilimo cha Pamba

Serikali Imewahakikishia Wakulima Wa Pamba Nchini Kuwa Itaendelea Kufuatilia Upatikanaji Wa Viuadudu Vya Zao La Pamba Na Kuhakikisha Vinawafikia Wakulima Kwa Wakati.

Naibu Waziri Wa Kilimo Hussein Bashe Ameyasema Hayo Tarehe 3 Februari 2020 Wakati Akijibu Swali La Mbunge Wa Jimbo La Geita Vijijini Joseph Kasheku Msukuma Aliyetaka Kufahamu Serikali Inampango Gani Kupeleka Dawa Za Kuuwa Wadudu Wa Pamba Kwani Zinazopatikana Huwa Ni Chache.

Bashe Amesema Kuwa Sehemu Ya Utekelezaji Wa Hamasa Za Kilimo Cha Pamba, Katika Msimu Wa Kilimo Wa Mwaka 2017/2018, Viuadudu Zenye Thamani Ya Shilingi Bilioni 16.8 Na Vinyunyizi 15,300 Vyenye Thamani Ya Shillingi Milioni 462 Vilinunuliwa Na Kusambazwa Mwaka Huo.

February 4, 2020

TCRA kuwabaini waliosajili kadi za simu kinyume na utaratibu
TCRA kuwabaini waliosajili kadi za simu kinyume na utaratibu

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kushirikiana na watoa huduma, imetangaza kufanya uhakiki wa laini zote za simu zilizosajiliwa ili kuondoa wale waliosajili kwa kutumia kitambulisho cha mtu mwingine ili kuwachukulia hatua za kisheria.

Kwa mujibu wa tangazo la mamlaka hiyo, TCRA imeamua kufikia uamuzi huo ili kujiridhisha kama waliosajili laini zao za simu wametumia kitambulisho sahihi.

Lakini Ofisa mwandamizi wa TCRA, hakufafanua ni lini uhakiki huo utaanza, huku akiendelea kusisitiza uzimaji wa laini ambazo hazijasajiliwa unaendelea.

January 28 2020

Hakuna Mtanzania mwenye virusi vya Corona
Hakuna Mtanzania mwenye virusi vya Corona

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi, amesema kuwa hakuna Mtanzania anayeishi nchini China, aliyekumbwa na maambukizi ya virusi vya homa ya Corona

Waziri Kabudi ameyasema hayo wakati akitoa ufafanuzi juu ya hali ya Watanzania waishio nchini China na kusema kuwa Tanzania ina wanafunzi elfu nne na katika mji wa Wuhan kuna wanafunzi 400 .

Amesema kuwa Tanzania kwa kushirikiana na balozi wa Tanzania Nchini China,Mbelwa Kairuki, wataendelea kufuatilia kwa ukaribu kujua maendeleo na hali za watanzania wanaoishi jimboni wuhani na china kwa ujumla,ila kwa sasa hakuna mtanzania aliyeathiriwa na ugonjwa wa korona.

January 28 2020

Manispaa ya Tabora Kupoteza mamillioni
Manispaa ya Tabora Kupoteza mamillioni

Halmashauri ya manispaa ya Tabora imepoteza zaidi ya shilling million mia tatu kutokana na ukusanyaji mbavu wa mapato

Licha ya manispaa ya Tabora kupanda katika ukusanyaji wa mapato bado kumekuwepo na upotevu wa mapato hayo kutokana na mfumo mbovu wa ukusanyaji wa mapato hali iliyosababisha Halmashauri ya manispaa ya Tabora kupoteza zaidi ya shilling million mia tatu.

Fedha hizo zimebainishwa kupotea katika kikao cha baraza la madiwani baada diwani wa kata ya tumbi bw Ellias Lucas Ndembele kuhoji juu ya mikakati iliyowekwa na serikali namna ya kukusanya mapato, hivyo akaomba kuainishiwa maeneo ambayo mapato yamepotea pamoja na kiasi cha fedha.

Baraza hizo la madiwani limepitisha bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2020/2021 ya shiliing billion 69 huku Baraza hilo la madiwani manispaa ya tabora likivunjwa rasmi hapo jana mpaka litakapoundwa upya

January 28 2020

TCRA Kuzima laini za simu awamu ya pili
TCRA Kuzima laini za simu awamu ya pili

Zoezi la uzimwaji wa line za simu ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole kwa awamu ya pili leo linaendelea nchini .

Mamlaka ya masiliano Tanzania imethibitisha hayo na kusema kuwa zoezi hilo ni endelevu na leo , zaidi ya watu milioni tatu watazimiwa laini zao za simu kwa makundi.

Kwa mujibu wa TCRA zoezi hili litachukua awamu kadhaa hadi kukamilika na kumaliza watu takribani milioni 20 wanaotumia Simu bila kujisajili kwa alama za vidole.

January 23, 2020

Wanafunzi Tabora Kusomea Usafiri wa Anga
Wanafunzi Tabora Kusomea Usafiri wa Anga

JUMLA ya wanafunzi mia tisa ( 900) wa Kidato cha Tano na Sita mchepuo wa Sayansi katika shule za sekondari tatu za Mkoani Tabora wamepewa elimu juu ya kujiunga na sekta ya usafiri wa Anga pindi watakapoliza shahada zao za vyuo vikuu.

Mafunzo hayo ya siku moja yamehusisha wanafunzi 500 wa Shule ya Sekondari ya Milambo, 200 WA Tabora Wavulana na 200 wa Tabora wasichana.

Baada ya mafunzo hayo, Afisa Habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini(TCAA) Bestina Magutu amesema lengo la elimu hiyo ni kuwasaidia wanafunzi wanasoma masomo ya sayansi kuwa na uelewa mpana na kuchangamkia fursa ya masomo yanayohusu sekta ya anga.

Bestina amesema lengo jingine ni kuwahamasisha ili waanze kujiandaa kwa ajili kusomea fani mbalimbali za sekta ya anga kama vile urubani , uongozaji ndege, ufundi wa ndege , usimamizi wa usalama wa usafiri wa anga na huduma kwa wateja.

January 23, 2020

Mifuko feki yataifishwa na serikali
Mifuko feki yataifishwa na serikali

Baraza la usimamizi na uhifazi wa mazingira NEMC limetaifisha mifuko mbadala isiyokidhi vigezo yenye thamani zaidi ya million tatu katika manispaa ya Tabora.

Katika ukaguzi wa kushitukiza uliofanyika katika maduka 8 yanayouza mifuko, maduka matano yamekutwa na mifuko hiyo ambapo mkaguzi wa mazingira kutoka NEMC kanda ya kati mhandisi Bonphas Paul Guni amesema mifuko hiyo imetaifishwa na watuhumiwa wote wamekili kulipa faini ya shilling laki sita na hamsini elfu.

Nao wauzaji wa mifuko hiyo isiyokidhi vigezo wamesema serikali ichukue jukumu la kudhibiti utengenezaji wa mifuko hiyo viwandani kutokana na wafanya biashara wengi kutoitambua mifuko halali na isiyoruhusiwa hali iliyowapelekea kuingia hasara isiyo ya lazima.

January 23, 2020

Rais Magufuli awaapisha Mabalozi wane
Rais Magufuli awaapisha Mabalozi wane

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, jana amewaapisha Mabalozi Wateule wanne watakaoiwakilisha Tanzania katika nchi za nje.

Mabolozi hao wanne waliyo apishwa leo hii ni pamoja na meja generally mstaafu Gaudensi Millanzi ameapishwa kuwa balozi wa Tanzania nchini afrika kusini,Dkt:Modesto kipilimba kuwa balozi wa Tanzania nchini Namibia lakini pia prof:Emmanueli mwaluko benaa kuwa balozi wa Tanzania nchini zimbambwe pamoja na Dkt:Bensoni bana kuwa balozi wa Tanzania nchini Nigeria hafla hiyo ya uapisho imefanyika leo ikulu Jijini Dar es salaam.

Rais Dkt: Magufuli amewaomba mabalozi hao kwenda kuiwakilisha vyema nchini ya Tanzania katika mataifa hayo na kuzingatia masilahi ya Taifa.

Kwa upande wake waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afirika mashariki Prof:Pallamagamba Kabudi amewataka mabalozi hao kufatiliya maeneo yote ambayo rais Magufuli alikubaliana na maraisi wenzake alipotembelea nchi hizo hivi karibuni.

January 15,2020

Dkt.Ndumbaro akutana na mwakilishi ( ICRC)
Dkt.Ndumbaro akutana na mwakilishi ( ICRC)

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu ( ICRC) katika Nchi za Tanzania,Kenya na Djibouti Bw. Olivier Dubois.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam,ambapo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua na kuthamini mchango wa ICRC katika utoaji wa huduma na misaada ya kibinadamu hapa nchini.

Amesisitiza kuwa Tanzania ikiwa ni mwanachama hai wa ICRC itaendelea kutimiza wajibu wake wa Kitaifa na Kimataifa na kwa kuzingatia Sheria za kimataifa zilizopo chini ya ICRC.

Kwa upande wake Bw. Olivier Dubois ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuishirikisha ICRC katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali hususani ile inayohusu utoaji wa misaada ya kibinadamu.

January 15,2020


Radio Uhai 94.1 FM Tabora Sauti ya Tumaini

© Radio Uhai